
NIKUJUE ZAIDI Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
NIKUJUE ZAIDI - Paul Clement
...
Nimesikia kuwa kukujua Wewe ndio chanzo cha amani
Nimesikia kuwa kukucha Wewe ndio chanzo cha akili.
Nimesikia kuwa kukutii Wewe kuna mema ya nchi
Nimesikia kuwa kukusifu Wewe juu yangu una keti
**HOOK**
Nipe neema Yako, nijaze na kweli Yako
Ondoa unyonge wangu, inua imani yangu
**Chorus *
Nifundishe Neno Lako, niongoze njia Zako
Nionyeshe pendo Lako nikujue zaidi, nikujue zaidi x2
Nimesikia tena kuwa We' ni Mwanzo
Na tena ni Mwisho.
Kwa kuwa naujua tu huu wangu mwanzo Kwako nitaujua mwisho
Nimesikia tena kuwa We' ni yote
Tena ndani ya yote
Hivyo natafuta kukujua Wewe
Ili niyajue yote
**Hook**
Nipe neema Yako
Nijaze na kweli Yako
Ondoa unyonge wangu
Inua imani yangu
*CHORUS**
Nifundishe Neno Lako, niongoze njia Zako Nionyeshe pendo Lako nikujue zaidi, nikujue zaidi x2
**Bridge**
Zaidi ya vyote nikujue zaidi x4