![Neema Yako](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/03/03/ef1b792703d248278e65893552f9dd3d.jpg)
Neema Yako Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2021
Lyrics
Neema Yako - Walter Chilambo
...
umenitoa mbali kusikojulikana
kwa neema yako isiyosemekana
umenitoa kule kusikojulikana
kwa upendo wako usiosemekana
ni muujiza me kufika hapa
ni muujiza me kuwa hai
ni muujiza kupendwa na wewe Yesu
ni muujiza kusimama tena
si kwamba Mimi nimetenda wema sana
si kwamba Mimi ni mtakatifu sana
si kwamba Mimi ni mnyenyekevu sana
si kwamba Mimi niko sawa sawa sawa sana
Ila ni neema yako Bwana
Ni neema yako Bwana
neema yako Baba
Musical Instrumental
duniani nimekutana na mengi
tabu na misukosuko, kuishiwa na kucheka
duniani nimepambana na vingi, kutengwa na kukataliwa
Mimi eeh, ninaona ajabu hukuniacha nilivyo
ajabu hukunipungukia Yesu
si kwamba mimi nimetenda wema sana
si kwamba Mimi ni mtakatifu sana
si kwamba Mimi ni mnyenyekevu sana
si kwamba Mimi niko sawa sawa sawa sana
ila ni neema yako Bwana
ni neema yako Baba
Ni neema yako Bwana
Ni neema yako Bwana
Ni muujiza
Yesu unaniwazia mema
mazuri unanitendea
ni muujiza