![Najivunia](https://source.boomplaymusic.com/group1/M0B/4D/2F/rBEezl13kM-AWQpxAAEnNtIP56k348.jpg)
Najivunia Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2019
Lyrics
Ningekuwa na mali
Magari ya kifari
Bila amani
Ninajivunia nini
Pesa nyingi
nyumba na biashara
Bila amani
Si mali kitu kama unaishi unalia ndani yako
Kwa maumivu tena umeshikilia imani zako
Wamsahau mungu eti unajivuna ni nguvu zako
Na shule umesoma tena unajidanganya ni akili zako.
Polee
Duniani sipakujivunia jina
Wala mavazi ya heshima
Bali neno la uzima
Litatuongoza vyemaaa
Mwezenu mimi jamanii, najivunia kuwa na yesu
Vya dunia nimeviacha mbali, najivunia kuwa na Yeye
Yesuu pekee yake anasimama, najivunia kuwa na Yesu
Mfalme wa wafalme, najivunia kuwa na yeye
Yeye ni mwalimu wa walimu
Ananifundisha vyema
Yeye ni tabibu wa karibu napata tiba njema
Yeye ni dereva ,anazijua njia zangu baba wo
Yeye ndie Shujaa anishindia vita yangu baba wo
Si mali kitu kama unaishi unalia ndani yako
Kwa maumivu tena umeshikilia imani zako
Wamsahau mungu eti unajivuna ni nguvu zako
Na shule umesoma tena unajidanganya ni akili zako
Polee
Duniani si pakujivunia jina
Wala mavazi ya heshima
Bali neno la uzima litatuongoza vyema
Mwenzenu mimi jamani, najivunia kuwa na yesu
Vya dunia nimeviacha mbali najivunia kuwa na yeye
Yesu pekee yake anasimama najivunia kuwa na Yesu
Mfalme wa wafalme najivunia kuwa na yeye
Kwa maana hii mungu, aliupenda ulimwengu
Akamtoa mwanae wa pekee, Ili kila mtu a mwaminie asipotee
Bali awe na uzima wa milele
Najivunia kuwa naye
Mwenzenu mimi jamani, najivunia kuwa na Yesu
Vya dunia nimeviacha mbali, najivunia kuwa na yeye
Yesu peke yake anasimama, najivunia kuwa na yesu
Ninatembea kwa maringo ngongongo, najivunia kuwa na yeye