Kijiba Lyrics
- Genre:Taarab
- Year of Release:2023
Lyrics
Kijiba - Jahazi Modern Taarab
...
Kimekukaeni kimekukaeni kooni kijiba cha roho
Kimkusakameni kimekusakameni kooni kijiba cha roho
Ya kwenu yamewashinda, ndio maana mnaumia roho
La ubani limeshavunda, kiwasakame kijiba cha roho
Kwani lipi linowaumiza, linowaumizaa
Hasa kipi kinowatatiza, kinowatatizaa
Kwani lipi linowaumiza, linowaumizaa
Hasa kiipi kinowatatiza, kinowatatizaa
Nawajua nyinyi watu, mna mambo zenu
Nimechagua nna utu, si khulka zenu
Nawajua nyinyi watu, mna mambo zenu
Nimechagua nna utu, si khulka zenu
Nikiharibikiwa roho zenu kwatu, hizo ndo zenu
Nikifanikiwa mashavu futu, mbaya roho zenu
Nikiharibikiwa roho zenu kwatu, hizo ndo zeenu
Nikifanikiwa mashavu futu, mbaya roho zeenu
Hamtaki mtu apate na afanikiwe, lazima roho mdate mchanganyikiwe
Hamtaki mtu apaate na afanikiwe, lazima roho mdate mchanganyikiwe
Mnakijiba cha kifyate, lazima muughumiwe
Mnakijiba cha kifyate, lazima muughumiwe
Mnakijiba cha kifyate, lazima muughumiwe
Mnakijiba cha kifyate lazima muughumiwe
Mnanikunjia nisipate, riziki kwangu isiwe isiwe
Mungu ni wa kwetu sote, kwetu sote
Kivipi yangu yasiwe, yasiwe
Oooooh! Mnanikujia nisipate, oooh! riziki kwangu isiwe isiwe
Aaaah Mungu ni wa kwetu sote, kwetu sote
Aaah! Kivipi yangu yasiwe, yasiwe
Mtakufa nachoo, kijiba cha roho
Na chenu kijicho, kitawala roho
Naona kinawachoma eeeh!, Kinawakereketa
Naona kinawachoma eeeh! Kinawakereketa
Oooooh! Naona kinawachoma eeeh! Kinawakereketa
Naona kinawachoma eeeeh! Kinawakereketa
Ukuukuu wa chuma eeeh! Sio upya wa boriti. Utajua hujui
Ukiujua huu ule huuwezi, utachoka miguu kwa utembezi bibi weee.
Upo nyonyo
Nawajua mambo zenu binadamu, kuwachukia wenzenu sina hamu.
Nawajua mambo zenu binadamu,
Kuwachukia wenzenu sina hamu.
Sina hamu na nyie enyi binadamu, kwanini mnichukie mie sina hamu.
Yangu mniharibie buree
Nawajua mambo zenu binadamu, kuwachukia wenzenu sina hamu.
Kunikazia ndio zenu niharibikiwe,
Mungu si mjomba wenu msijisumbue
Mkaacha mambo yenu buree
Nawajua mambo zenu binadamu,
Kuwachukia wenzenu sina hamu.