![Njia ya Msalaba](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/05/08/a93a94946d0f41bdbbe43fd80d299ef8_464_464.jpg)
Njia ya Msalaba Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Njia ya Msalaba - Catholic Church Songs
...
* * * * * *
Umekosa Nini we Yesu, kushtakiwa bure kwa Pilato
Wenye kustahili hukumu, si wewe, si wewe, Bwana ni sisi
Ole msalaba huo mzito, apagazwa Mwana Mpenzi wa Mungu
Mwili waenea mateso, alipa, alipa madhambi yetu
Ona Mumba Mbingu na nchi, yupo chini mzigo wamwelemea
Na mtu kiumbe chake kwa ukali, ampiga, ampiga bila huruma
Huko njiani we Maria, waonaje hali ya mwanao
Ni damu tupu na vidonda, machozi, machozi yamfumba macho
Kwa Simoni heri ya kweli, mimi pia Yesu nisaidie
Kuchukua mzigo wa ukombozi, kuteswa, kuteswa pamoja nawe
Uso wa Yesu malaika, Bethlehemu wakuabudu
Bahati yake Veronika, kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu
Wakimvuta huku na huku, wauaji wakamchokesha bure
Chini wamtupa bado kwa nguvu, aibu, aibu yao milele
Wanawake wa Israeli, msilie kwa sababu hiyo
Muwalilie hao kwa dhambi, upanga, upanga ni juu yao
Mwokozi sasa ni ya tatu, kuanguka chini ya msalaba
Katika dhambi za ulegevu, nijue, nijue kutubu hima
Muje malaika wa Mbingu, funikeni mwiliwe kwa huruma
Vidonda vyake na utupu, askari, askari wamvulia
Hapo mkristu ushike moyo, Bwana wako alazwa msalabani
Mara miguu na mikono, yafungwa, yafungwa kwa misumari
Yesu mpenzi nakuabudu, msalabani unapohangaika
Nchi yatetemeka kwa hofu, na jua, na jua linafifia
Mama Maria mtakatifu, upokee maiti ya mwanao
Tumemwua kwa dhambi zetu, twatubu, twatubu kwake na kwako
Pamoja naye kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo
Yesu tuwe wakristu wa kweli, twakupa, twakupa sasa mapendo
* * * * * * * * *
Katika roho yangu Bwana, chora mateso niliyokutesa
Nisiyasahau madeni, na kazi, na kazi ya kuokoa
sauti za kuimba | paneli la kiswahili
gafkosoft © 2025