
Sauti Ya Watu Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Sauti Ya Watu - Nay Wa Mitego
...
Hii sio sauti ya kiharakati
Wala ukombozi wa musa na fimbo yake
Bali haya ni maumivu ya mnyonge
Anaewakilisha walala hoi wenzake
Kwenye kinywa kilichokosa pakuseme hisia zake
Mmmh eee mmh eee mmm eeeh
Rais
Natanguliza samahni kwa wale ntakao wakwaza
Yamenifika hapa nimeshindwa kunyamaza
Wapo wengi kama mimi wenye sauti kama mimi
Sijui ni ubinafsi hawasemi kama mimi
Anko alisema kwamba tupo uchumi wakati
Haya tudanganyeni tena tupo uchumi wangapi
Wapigaji walotumbuliwa ndo wamerudi mzigoni
Kamladi kwa million mnataja mabillion
Hamna huruma nyinyi na sisi masikini
Hivi hiyo bajet si mngeweka hosptalin
Na huyu ndo yule binti aliemaliza chuo bila uwakika wa kazi alosomea huko chuo
Hajui atafanya nini amebaki na vyeti vyake
Anajuta alisoma nini si angejiuza ka wenzake
Panya road jina la pili la kijana asiekua na ajira
Na risasi ndo hukumu inayomfika ata asie na hatia
Huna afadhali wa maisha vyuma vimezidi kukaza
Mambo yanaharibika na wapinzani wamenyamaza
Kama ulimpenda baba huwezi muelewa mama
Na kama hukumpenda baba bado utamchukia mama
Yani kumpenda mama na kumchukia baba
Ni sawa kuipenda nyama alafu hupendi mchuzi wake
Mmmh eeeh
Mmh hii ni sauti ya watu
Na hilii giza tunaenda wapi
Tunafanya nini
Tutaishi vipi
Ata mwanga hauonekani
Mmmh eeh mmh eeh mmmh eeh
Ukiona mtoto halii njaa na nyumbani hakuna chakula
We mchunguze vizuri kuna sehem anakula
Hii ni kweli mama hali mbaya sio tandale sio masaki
Kilio chakila mtu pesa hakuna imefichwa wapi
Sikuhizi mpka vigenge vya nyanya TRA wanataka kodi
Masikin amejichanga vipesa bank anakatwa tozo
Hivyo V8 mnavyonunua si hela zetu za kodi
Naona mnaenjoy kuliko ata walipa kodi
Mnajenga hosptal madawa hakuna
Mnatujengea shule lakin walimu hatuna
Kudanga ndo kimbilio kubwa la wadada zetu
Ndo mtaji asokopeshwa hakatwi tozo wala kodi
Hivi mna akili nyinyi mnashauri tujiajiri
Wakati nyinyi wenyewe mpka sasa umeajiliwa
Acheni nafasi zenu na nyinyi mkajiajiri
Hapo ndipo tutakapo amini kweli nyie washauri wazuri
Kati ya mtawala na mpinzani
hapa muoga nani
Mtawala aliekataza mikutano isifanyike
Au mpinzani asiefanya na anajua ni haki yake
Mmh hii ni sauti ya watu
Na hili giza tunaenda wapi
Tunafanya nini
Tutaishi vipi
Ata mwanga hauonekani
Mmmh eeh mmmh eeeh mmmh eeh
Heheh bi mkubwa anapambana sana
Pengine hofu ni kuhusu swali la msingi
Kwenye vijiwe vyetu
Je vita yake na anaowaamin ni sawa
Isije ikawa ni mbinu tofauti
Heh tumerudi kule kule
Maji ya mgao umeme wa mgao
Maji hayatoki bili zinatoka
Mmh police hongereni kwa jitihada nyingi
Amsemi kwa ubaya lakini pia hamsingiziwi
Acha iendelee kunyesha tuone panapovuja
Mmh eeh mmh eeh mmh eeh mmh eeh