Intro ft. Sky Walker
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2021
Lyrics
Intro ft. Sky Walker - Stamina (TZ)
...
sauti yako kuitoa baada yakuuona mwanga wa dunia kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kilio chenye sauti nyembamba na kali masikioni ilikuwa ni furaha iliyoambatana na machozi yaliochuruzika kutoka machoni mwa mama yako alipokushika kwa mara ya kwanza ukiwa kichanga kidunchu na so innocent licha ya kuirithi dhambi ya asili toka kwa adam na hawa kama maandiko yanavyosema ikawa mwezi ikawa mwaka siku ya kwanza unatamka (mama) mamaako alimngoja kwa hamu kubwa mumewe arejee toka kazini amsimulie na wafurahi pamoja siku uliposimama ulipotembea hali iliuwa ile ile siku wanakupeleka shuleni kwa mara ya kwanza hali ilikuwa ile ile pia furaha tele shuleni ukakutana na mazingira mapya marafiki wapya wazuri na wabaya pia haikuchelewa kesi zikaanza kuwafikia wazazi mara umempiga jiwe mtoto wa mtaa wa pili mara umevunja kioo cha gari la mtu basi tabu tupu kwa mara ya kwanza ukamshuhudia baba yako akiwa na hasira kama mbogo akakutandika sawasawa ujana ulipopiga hodi vurugu nazo zikawa mara dufu sekondari ukaimaliza kwa mbinde pombe bangi mademu vilikuwa sehemu ya menyu kwenye sinia la maisha yako enzi hizo ukawapa wazazi mjukuu wao mapema japo ukamuachia mzigo mamae ambae ilibidi aache masomo kumlea wewe hukujali ukasonga mbele baada ya kuwafedhehesha wazazi kwa pilikapilika nyingi za ujana hatimaye ukawapa furaha tena ukiwa umevalia joho ukahitimu chuo muda wa kujitegemea ukafika wazazi wakasitisha kukupa pocket money hapo ndipo ukauelewa msemo usemao kuwa uyaone maisha ukayaona yakakupiga ukayawezea tena baada ya kupata kazi hamu yakuwa na familia ikapamba moto ukapata mke mzuri akakuzalia watoto ndoa ilikuwa tamu na wakati mwingine ilikuwa chungu maisha ya upendo uliyoyaona kwa wazazi wako yakakupa ujasiri na uvumilivu maisha yakakimbia kwa kasi ikafika wakati wako kuwalea wazazi dunia ikakupa pigo moja baada ya jingine ukamzika baba na juzi tu umemzika mama kuondoka kwa mama yako kipenzi kumekufanya uione dunia kuwa ni jitu fulani katili mno pigo hilo limekupa funzo pia kifo kipo na kila mtu ndio mwisho wake swali ni baada ya kifo umejiandaa kwenda wapi? jehanam au paradiso kumbuka maisha yako ya sasa yataamua sehemu utakayoishia hii ni paradiso by stamina
Similar Songs
More from Stamina Shorwebwenzi
Listen to Stamina Shorwebwenzi Intro ft. Sky Walker MP3 song. Intro ft. Sky Walker song from album Paradiso is released in 2021. The duration of song is 00:02:59. The song is sung by Stamina Shorwebwenzi.
Related Tags: Intro ft. Sky Walker, Intro ft. Sky Walker song, Intro ft. Sky Walker MP3 song, Intro ft. Sky Walker MP3, download Intro ft. Sky Walker song, Intro ft. Sky Walker song, Paradiso Intro ft. Sky Walker song, Intro ft. Sky Walker song by Stamina Shorwebwenzi, Intro ft. Sky Walker song download, download Intro ft. Sky Walker MP3 song
Comments (66)
New Comments(66)
MbalaiElisha
Azora32b4a
❤️
152814013
nakubl big up san
yusuph mwanjalali0jdtz
Nzuri sana brother
naqubal
kaz nzur broo.only one rapa
Asha omarydcxia
[0x1f627][0x1f60e][0x1f636]
Lorraine Mike
pull up
Farid Amanzifijh4
boom
James Mapande
nice
139062797
jo jhud loaYya phire usny la daony7
daaaah good xmx
139062797
job ho ryyo bta dson. mujhy
[0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f][0x1f63f]
Nice blaza