Mwenyewe Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Mwenyewe - Jessie
...
Hali yangu inazidi kuwa taabani,
We ni halali yangu,
Iweje mapenzi unipimie kwa mizani,
Yani penzi langu lanigeuza hayawani,
We kabali yangu,
Ila mapenzi ya kushare mi nitamtambia nani?
We hunijali nachoshwa,
Sa vipi penzi liendelee?
kitu gani unakosa?
Sema nami nijitetee.
Unanifanya kufuri,
Nilinde nyumba usiku ukitoka eeh!
Na ukirudi kiburi,
Nina moyo wa nyama mi nimechoka eeh.
Nitabaki Mwenyewe
Acha nibaki Mwenyewe
Nitabaki Mwenyewe
Acha nibaki Mwenyewe
Text alfajiri kujibu alasiri
Dharau gani yeah..
Mbona nakujali, najali yako hali we huthamini
Shubiri hailambwi,
Yamekuwa moto mapenzi yanitese,
kama kuachana dhambi
so kwa hili joto iyo pepo niikose
Bila mawingu mvua imenyesha,
Ndo kwanza hunielewi weee
Unafanya kunikomesha
Amani nikose hee...
Unanifanya kufuri,
Nilinde nyumba usiku ukitoka eeh!
Na ukirudi kiburi,
Nina moyo wa nyama mi nimechoka eeh.
Nitabaki Mwenyewe
Acha nibaki Mwenyewe
Nitabaki Mwenyewe
Acha nibaki Mwenyewe
Wanaokutamani wengi baba unawindwa,
ila jua mwangu moyoni wewe unapendwa...
Huenda sina sura, ila moyo wa kupenda ninao
We baki na vigagura, najitoa msafara wao.
Nitabaki Mwenyewe
(Mwenyewe ntabakiaaa aah)
Acha nibaki Mwenyewe
(Mwenyewe yeeahh)
Nitabaki Mwenyewe
(Mwenyewe , Mwenyewe hey hey)
Acha nibaki Mwenyewe