Pingu Za Maisha ft. Murathe Ngigi, Liboi, Lexas Mshairi, Karembo & Kikete FM Lyrics
- Genre:Spoken Word
- Year of Release:2021
Lyrics
Ma-stars ni watu wana scars
Napenda kuvaa kushinda venye napenda issues kuzi address
Napenda madem lakini hao pia ukikosa pesa ni stress
Life kwangu ni ngori
Nimezoea noma hadi ukiwa mpole naona wewe ni fala
Napenda kuvaa ma-CAT
Ata kama nafika tu bei ya Akala
Napenda ma-silver lakini sina ma-coins
Nnapenda ma pete lakini sijaoa
Ju pingu za maisha kwangu ni kitu tofauti
Ju crime kwa mgongo ya mtaa yangu ndo uti
Pingu za maisha
Zinatuchanganyisha
Tunadhulumiwa
Ni lini yataisha?
Nipe funguo
Nihepe kituo
Nione ufuo oooh...
Nilipenda foota
As well nilipenda mbuta
Nikitoka grao hio ndio place ungenikuta
Funny enough mamako alikua anasaidia mamake kuziuza
Day after day hivo ndio uhusiano wetu tukaukuza
Mwezi moja into it maulana wewe akatutuza
Mamangu akapata rumors but hakuwa sure
Nikafika kum-break-ia news juu baba hakua
Naye akajua
Akatupa baraka
Na hivo haraka mi na mathako tukakua one
Jua hivi ukiwa tumboni my son
Kufa ni rahisi, kuishi ndio ngumu zaidi
Hizi kumbukumbu najitahidi kuzikumbuka
Mbele yangu pakiwa na bunduki
Karao aki-insist mi ni mamluki
Juu nikona dredi
Mnato wa lugha yangu haupendi
Nafaa nidedi
Juu nafanana wenye upora watu wikendi na magizani
Na hivo yaani
Ndio akafinya trigger
Of late na-smile then na-frown
Niko kwa pool ya mawazo na the more I think the more I drown
Me husoma bible but huezi ni-convince ati hii ni good news
I mean am just 15 years and am expectant
Nangoja 9 months ziishe ndo ni-push
But sidhani ka niko na nguvu ya ku-push through those months of depression
Mshaanza ku-notice some changes from outside
But hamjui on the inside there is something growing
Adding weight and losing shape
Babybump isha-pop
Wanakijiji wanadhani sikutii wazazi
Hawajui kuwaskiziza ndo imenifikisha hapa
Kukumbuka vile boy wangu alimadwa
Kukumbuka the last time I touched his lips
And this time round they were not kissing me
They were saying his last words as he touched my belly
Here I have the love of my life
Lying on my chest with blood all over his body
And my young king inside my belly knocking
Waiting for the day I'll open this door for him
Natamani kukata maji nikue high ni-escape
But it's too late mtoi amekata maji mbele yangu
Pingu za maisha
Zinatuchanganyisha
Tunadhulumiwa
Ni lini yataisha?
Nipe funguo
Nihepe kituo
Nione ufuo oooh...
Nikiwaza naona huyo boy akiingiza huyo dame box
Na baadaye anamwingiza pia kwa shanty
Hapo ndio Ghetto love inamea roots
Juu reggae kwa woofer inamaanisha party
One month later ha-buy pads akiwa shopping
Arrival yangu ni apparent
Baba kuambia mathake that soon atakuwa grandparent
Mukuru naye kuangalia juu na kuambia Mungu asante
Mjukuu ni backup juu long life kwa boychild ghetto ni uncertain
Hivyo ndio matha na baba wanaanza kuishi pamoja
Kila time baba akitoka kwenda kandarasi
Na-sense wasiwasi kwa matha
Kila siku maombi kwa Jah Jah
Amweke safe mpaka jioni tuwe sote together
Seems ripper aliita na jina lake likawa next kwa orodha
Father to be ashageuka fodder to a policeman's bullet
So watoto wengine wakiandika juu ya baba zao shule
Yangu itakuwa tu ni blank page kwa kitabu
Juu birthdate yangu imekuja
Two months too late
Ilikuaje baba akaaga
Kabla kuzaliwa kwa mwana
Ni Maulana au ni ibilisi alipanga?
Labda hamna zaidi ya jua
Likitua
Kaburi giza
Kiburi lala salama
Mwili inageuka
Chakula cha mchwa
Au labda mama na majamaa
Watamweleza mwana
Wakiiga maoni ya baba
Kama mimi mfano
Wa vile hufai ufanye
Usifwate nyayo
We fuata moyo
Kula vibes za minds na pages
Your moves zi-grow wings za sages
Chora ujanja ya bob
Lenga picha mob
Ju hata smiles za selfies
Huficha struggles on the Margins
Brathe
Jenga name na keja
Manze
Chunga kuhanya na liquor
Gathe
Hakuna mercy for the species
Kwa hizi street hustles
Cheki niliangushwa na risasi
Hadharani kwa roadi
Na mwizi anajidai polisi
Akidai mimi ndio pwaguzi
Lazima nikatizwe pumzi
Maybe hii seed generation
From your mum
And I is consummation
Ndio itakua redemption
Ya protégé wa ma alleyways
For zile sins
Haziwezi make-it kwa eulogies
Pingu za maisha
Zinatuchanganyisha
Tunadhulumiwa
Ni lini yataisha?
Nipe funguo
Nihepe kituo
Nione ufuo oooh...