O Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2023
Lyrics
IKO WAPI-NIMPHIL PAUL - Nimphil paul
...
Nahisi nimetwikwa msalaba,
wakunitua simuoni,
kidume nimekosa kaba,
yamenifika shingoni,
haba zangu hazijazi kibaba,
nachokitafuta sikioni,
hali ya maisha chechema ka chiba,
Alfajiri kokoriko,
naamka na masikitiko,
nawaza niende miangaiko,
nikasake salale,
yanatimia nusu maandiko,
natokwa jasho. sipati diko,
tumbo nalo halina likizo,
Kila siku ladai,
Yarabi Mola ninusuru,
dhiki zimenipa kata,
najipa Imani nimapanga msururu,
ningoje wapate nitafwata,
hali yanizidi nataka kufuru,
maana sipati kitu na jasho lantoka,
ety kama ndege na sifa ya kunguru,
havinifai vitamu, yangu mizoga,
Iko wapi,
Iko wapi,riziki yangu,
Iko wapi, furaha yangu,
Iko wapi , riziki yangu ,
Iko wapi furaha yangu ,
Inachosha jua navyosota,
alafu nambulia mikono mitupu,
vyakula vyangu sili vya mafuta,
nameza vilivyo chukuchuku,
mie wa mchicha ni mchicha tu,
hata nikila nyama ni mapupu,
ewe baba Mungu uketie juu,
niepue kwenye shimo la ukapuku,
Nimechoka ,
tamaa nimekata,
natamani akufa,
niziepuke shida hizi,
nimedhohofika,
najikokota,
mbwa natapatapa,
imenipiteza miluzi,
Yarabi Mola ninusuru ,
dhiki zimenipa kata ,
najipa Imani nimapanga msururu,
ningoje wapate nitafwata ,
hali yanizidi nataka kufuru,
maana sipati kitu na jasho lantoka ,
ety kama ndege na sifa ya kunguru
havinifai vitamu yangu mizoga,
Iko wapi,
Iko wapi, riziki yangu,
Iko wapi, furaha yangu,
Iko wapi ,
Iko wapi ,(mbona najituma), riziki yangu,
Iko wapi, furaha yangu,