Nikubali Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
[Intro]
Pekee naomba unikubali Bwana,
Hakika katika maisha yangu.
Pengine wanadamu, wanaweza wasinifae kuna wakati,lakini nikiwa na wewe Bwana naamini nitakuwa salama.Nikubali Bwana!
[Chorus]
Nikubali niwe wako
Mboni yangu iwe ni wewe 2x
[Bridge]
Nikubali
Niwe wako 2x
[Stanza 1]
Kama mvua inyeshavyo kweli
Toka juu kuja chini
Naziona na baraka zangu
Zaja ukinikubali
Mbele zako nasogea bwana
(Mbele zako nasogea)
Ombi langu nikubali Bwana
Maisha yangu mtihani sana(sana)
Yanatisha kama nini(nini)
Ila wewe ndani yangu Bwana(Bwana)
Kila siku najiamini(mini)
Usiniache gizani Bwana
Nitakosa msaada Bwana
Mabonde mabonde ondoa(ondoa)
Visiki visiki ondoa(ondoa)
Mizizi ya shetani ondoa(ondoa)
Nataka iwe amani (amani)
Mabonde mabonde ondoa(ondoa)
Visiki visiki ondoa(ondoa)
Mizizi ya shetani ondoa(ondoa)
Moyo wangu Bwana ukusifu wewe
[Bridge]
Nikubali
Niwe wako 2x
[Chorus]
Nikubali niwe wako
Mboni yangu iwe ni wewe
2x
[Bridge]
Nikubali
Niwe wako 2x
[Stanza 2]
Mwanzo Bwana wangu(Bwana wangu) Ulinipenda
Msalabani ukanifia
Wewe ndiyo ngome yangu
(ngome yangu) iliyo njema
Uweponi mwako nabarikiwa
Ulinitoa matopeni
(Ukaniweka juu juu juu)
Naomba nami unikubali
(Niwe wako tu tu tu)
Kuna wakati Messiah
Nashindwa kuielewa nafsi yangu
Mbele zako nikisogea
Mawazo yanatawala akili yangu
Lakini badooo
Bwana u mwokozi wangu
{Japo kidogo} nakukosea
Niponye na huu udhaifu wangu
Bwanaaa
[Bridge]
Nikubali
Niwe wako 2x
[Chorus]
Nikubali niwe wako
Mboni yangu iwe ni wewe 2x
[Bridge]
Nikubali
Niwe wako 2x
[Stanza 3]
Nasogea kwako
Bwana nimekuja kwako
(Kutafta msaada) 2x
iiih! Mimi kama Mimi siwezi
Nahitaji msaada wako 2x
[Outro]
Nikubali(Bwana nikubali wewe)
Niwe wako(Jehova nikubali)
Nikubali(Niwe wako)
Niwe wako
Oooh YESU nikubali
(Kahama Quality Studio
Studio ya ukweli)