Ghetto Remix (feat. Tway 360) Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2022
Lyrics
[into]
Mara kokoriko jogoo anawika
Pamekucha mawio
Kweupe kwa jiko
Hakuna cha kipolo wala masalio
Ghetto langu mwiko
Sitaki wageni nawakimbia mbio wowoh
Maana hata diko la kupika sina
Kila kitu ni zero
Mmyeeh, sebule ndio chumba godoro sakafuni
Kochi moja la babu yangu mzee wa kale
Yote tisa muumba hili hapa la kumi
Napopikia napolala ni palepale
Mara hodi-hodi mwenye nyumba anadai chake
Kama sina kodi ama zangu ama zake
Nishaweka bondi mpaka na vyombo pesa nipate
Sina kalamu ya wino maisha naandikia mate
Mamah mamah! Mamah! Weeh
GHETTO mmh,
GHETTO owoh woh woh woh woh
GHETTO maisha ya ghetto sio poa
Sio siri GHETTO, Ya maji bili nadaiwa
GHETTO baada sana mi kuoa
(Tway!!)
Ghetto langu ila sina raha (ghettoo)
Magetoni mi nalala njaa (gheettoo)
Ndani mafuriko ishatoboka paa (ghetto)
Maisha ya ghetto sio poa
Maisha sio poa yani bado najichanga changa
Kabati,vyombo ndani hakuna naisoma namba
Naganda-ganda majirani some times naonekana muhanga
Maana hakuna hata choo bafu lenyewe la kubuni-buni
Nina godoro ila kitanda changu sakafuni
Na nguo ndio ila kabati langu kwa kapuni
Magetoni na kideo chogo najivunia ndo mali yangu
hata ikiwa ndogo ndo ninayochekia mechi na wanangu
Mihogo ndo menyu kuu mixer na chachandu
ile mikogo ("tway nataka chips") sorry marufuku kwangu
Mara hodi-hodi mwenye nyumba anadai chake
Kama sina kodi ama zangu ama zake
Nishaweka bondi mpaka na vyombo pesa nipate
Sina kalamu ya wino maisha naandikia mate
Mamah-mamah-mamah weeh
GHETTO, mmh
GHETTO, owoh woh woh woh woh
GHETTO, maisha ya ghetto sio poa
Sio siri GHETTO, ya maji bili nadaiwa
GHETTO bado sana mi kuoa
Yeah! Denooz!
an icon with a marvelous tone!
____________________________________________________