Bwana Lyrics
- Genre:Spirituals
- Year of Release:2022
Lyrics
Nampenda yeye,
Sitomuacha kamwe,
Amenipenda mi,
Tangu kuzaliwa
Katika majonzi yangu,
Alinipa faraja aah!
Nilikuwa mkiwa, marafiki hakuna,
Hakunitupa
Nimlipe nini
Kwa aliyonitendea
Upendo wake kwangu haupimiki
Kutwa unajirudia
Nimlipe nini
Kwa aliyonitendea
Baraka zake kwangu hazikauki
Zinazidi kuchipua
Bwana Bwana Bwana
(Hakuna kama wewe)
Bwana Bwana Bwana
(Mwenye enzi yako)
....
Nilikuwa Misri,
Farao alinitesa,
Siku hazikuwa rahisi,
Kwa njia niliyochagua
Sasa nina amani, nina amani
Nimepona kwenye safari, kwenye safari
Acha niringe kidogo ooooh
Amenishika mkono ooooh-hoooh!
Bwana Bwana Bwana
(Hakuna kama wewe)
Bwana Bwana Bwana
(Mwenye enzi yako)
.....
Nikipatwa na shaka kimbilio ni YESU,
Kodi ya nyumba hailipwi kimbilio ni YESU,
Vita vya ndugu kwa ndugu kimbilio ni YESU
Ma-wifi kukusimanga kimbilio ni YESU.. ni YESU huyoo