
Pure Namba ft. Maulo Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2012
Lyrics
Pure Namba ft. Maulo - One The Incredible
...
(Verse 1)
yap yeah yeah
aah M rap tell me(M rap in the house)
mokoo aahh Dup touch(yeah),asante
Aah beat kali haifai bila vocal
daily nakula dry niko high kama popo
fanya worldwide sio ku-try kama local
fake MC ukijikoki me nasqueeze kama fofo
Aah verse baridi vaa koti,
salamu kwa wanangu wote sina ripoti
bado mishemishe support mwanangu Oppi
kila beat natoboa kama juice ya kijoti
me discipliner nawasimamisha wima
me nyaraka mpaka sura kama simu ya kichina
mistari na vina,kwenye shari habari sina
mchaga halali macho kwenye sarali daima
zunguka Kote hauna rafiki kama noti
sister-do hauna mnafiki kama shosti
tafta dili uza ata pipi we bitozi
tafta njia haya maisha hayamuliki kama tochi
(chorus)
(chap chap chap chap ni sawa
M rap pure math,rap ni dawa
chap chap chap chap ni sawa
pure mathematics, dogo utapagawa)×2
( Verse 2)
Aah yeah,we unachana me nachana mpaka basi
niko booth nina bick,karama na karatasi
sina hofu ninaspeak salama kwa sara safi
ila ukinivaa vibaya nakuchana kama vazi
sanaa,gharama haramuchati
harakati hii kubwa hupaswi simama kati
Verse inacheza judo,kata na sarakasi
baba mama m'barikiwe kusimama ka' wazazi
pure namba,hapa zinajamba zakubuni
mshamba kawa mjanja,mjanja ana ujanja wa kihuni
banja kwenye beat weka ladha ya sabuni
we ni base 10 log me namba ya kirumi
hii ni classic hata isipotamba kama Do me
kasi ya marapper inasanda kama uchumi
nina punchline na kick kama chuo kikuu cha ngumi
pure mathematics sina banda nna kampuni so
(Chorus)
(chap chap chap chap ni sawa
M rap pure math,rap ni dawa
chap chap chap chap ni sawa
pure mathematics dogo utapagawa)×2
(Verse 3)
kuna rapper mwenye akili na rapper batili
rapper anaepata kisaka na asiepata kisaka dili
tofauti kati ya rapper wa kwanza na rapper wapili
wa pili anataka umaster huku hajapata umahiri
fungua kurasa kwenye darasa la hip hop
somo halisi tunaoandika kuskika inataka promo
midomo inaskika ikisema na mikono inashika makoleo na kuzika waliomo
waliopotea njia wanataka kurudi nyuma
wapotovu wamechuna,waovu wamenuna inawauma
wamepoteza muelekeo,maendeleo yamegota watafanya nini leo
panapo matatizo tunataka suruhisho
likizo inawekwa kando,tunakaza mpaka kifo
na tulivyo,sio watu wa matambiko
tumeshaiteka kambi na kupekua maficho so
(yeeiii)
(Chorus)
(chap chap chap chap ni sawa
M rap,pure math rap ni dawa
chap chap chap chap ni sawa
pure mathematics,dogo utapagawa)×2
~kibs_traveller added this~