Kidudu Mtu ft. Baby J Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2017
Lyrics
Kidudu Mtu ft. Baby J - Offside Trick
...
Haiya haiya kidudu mtu
Haiya haiya kidudu mtu
Unafitinisha wenzako we hujali utu
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Kidudu kidudu gani usie tulia
Una maneno machafu watupakazia
Kidudu kidudu gani usie tulia
Una maneno machafu watupakazia
Imefika siku yako yaku simuliwa
Maisha yako ya nyuma yalipoanziaaa
Acha usutwe sutwe hujakoma wewe kidudu mtu
Yako yanakushinda ni hodari tu kusema ya watu
Hizo ni sifa mbaya jali utu wewe kuliko kitu
Hutoishi na watu roho yako chafu safisha kutu
Haiya haiya kidudu mtu
Haiya haiya kidudu mtu
Unafitinisha wenzako we hujali utu
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Ulikuja kwa uzuri tukakupokea
Tukakuona wa maana kumbe ni mmbea
Ulikuja kwa uzuri tukakupokea
Tukakuona wa maana kumbe ni mmbea
Mimi ni kama bahari ukinichafua
Nadondosha meli kubwa seuze ngalawa
Haiya haiya kidudu mtu
Haiya haiya kidudu mtu
Unafitinisha wenzako we hujali utu
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Wacha kula mapema kidudu mtu jiangalie
Hapo! Hapo!
Hapo! Hapo!
Offside Trick watoto wa ki-Zanzibari wakali wa hizi kazi
Umeskia wapi superstar anakula kwa mama ntilie?
Superstar anakula Kempinski bwana! Utafungwa
Wape vidonge vyao dada
Jamani eee!
Maisha ni kutafuta na sio kutafutana babu ee
Wenzako wanaomba kazi wewe unaomba pesa
Asiohaya wala hajui vibaya
Mvalisheni dira sasa pamoja na chupi ya bambino hei!
Yako hilo babu!
Watakuchun' babu mmm-mmwah
Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho
Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio
Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho
Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio
Hapo! Hapo!
Hapo! Hapo!
Hapo! Hapo!
Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho
Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio
Vitu vidogo vidogo vinakutoa roho
Vijimambo vidogo vidogo vinakuendesha mbio