Ametoroshwa Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2017
Lyrics
Ametoroshwa - Bizman
...
Uuuuh lalala Uuuuuuuh
(Instrumentals)
CHORUS:
Mimi mwenzenu, nasikitika sana
Ametoroshwa mpenzi wangu, nina uchungu sana Ameniacha nateseka, nasikitika sana
Sina hata la kufanya, nahangaika sana
Verse 1:
Wa moyo wangu unilipenda sana
Nasema tena nilipenda sana
Wahenga walisema
"Umdhaniae ndiye kumbe siye"
Na leo naamini
Yamenitokea kweli najuta aaah
Nilipokuwa na kazi nzuri, nilimtimizia mahitaji yote
Sasa kazi nimekukufa, mpenzi hanitaki tena
Kumbe alijali sana pesa, mimi hakunipenda tena
Tulipata mgeni mmoja, alinidanganya ni kaka yake
Tena nilimkaribisha, na nyumbani kwangu akalala
Akala msosi wa nguvu, pombe kibao nazo akanywa
Akanipa salamu nyingi, kutoka nyumbani kwa wazee
Pia akalalamika sana, eti kwa nini hapendi kuasalimu wazee
Nilimpa heshima zote, nikijua ni shemeji yangu
Kumbe alikuwa ni mwizi huyo ooooh, MASIKINI!
CHORUS:
Mimi mwenzenu, nasikitika sana
Ametoroshwa mpenzi wangu, nina uchungu sana Ameniacha nateseka, nasikitika sana
Sina hata la kufanya, nahangaika sana
Verse 2:
Siku ilipowadia, mimi sijui nini walalile
Mpenzi wangu anilitaka, twende bafuni tukaoge
Nilimkubalia mpenzi wangu, sikujua kinachoendelea
Nilivyoanza kuoga tu, mpenzi alinitaka radhi
Akaniambia amesahau, kutia maji kwenye mboga
Akabeba na taulo langu, nikabaki nilivyozaliwa
Akautumia muda huo, kutoroka na mpenzi wangu
Nikawaomba majirani, wanisaidie nikisikiie
Nilivyofika ndani kwangu, nikawakuta wameondoka
CHOOONDE! CHONDE CHONDE jamani CHONDE
Nawaomba msiwatoroke, wapenzi we ndo ni vibaya mno
Sina hata wa kunisaidia aaah
CHORUS:
Mimi mwenzenu, nasikitika sana
Ametoroshwa mpenzi wangu, nina uchungu sana Ameniacha nateseka, nasikitika sana
Sina hata la kufanya, nahangaika sana
(Instrumentals)
(OUTRO)
Nawaomba tuwe na mapenzi ya kweli (kumtoroka mwenzio)
Nawaomba tuwe na mapenzi ya kweli (sio vizuri)
Nawaomba tuwe na mapenzi ya kweli (Mapenzi Ya Kweli)
Nawatakia tuwe na mapenzi ya kweli
MAPENZI YA KWELI OOOOOOOOH WOOOOOAAH!