Usafi Ndo Deen (Remix) Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2022
Lyrics
Mbona wachafua mji
Weka kwenye bin
Weka kwenye bin
Nidhafu iwe ndo maadili
Usafi ndo deen
Usafi ndo deen
Uchafu punguza
Rudia tumia
Au zungushaa
Kitupa ovyo taka
Imani yaondosha
Tafadhali achaa
Maneno haya sote tuyakariri
Si watoto tu, hata na marijali
Tuzungushe taka tunapotumia
Tutenganishe taka panapotakiwa
Ma glassi
Karatasi
Na plastic
Na ta'ami
Tumia ya njano bin
Tupa kwa blue bin
Tumia nyekundu bin
Tumia kijani
Yasiende kwenye moja tu bin
Hebu anza leo
Hujachelewa
Jukumu n letu sote
Leo kesho mda wote
Daima tutalibeba
Jukumu n letu sote
Leo kesho mda wote
Daima tutalibeba
Una nafasi ya kusaidia mji wa Zanzibar
Mara kiatu chaganda kwa bubble gum
Wateleza kwenye maganda ya utam
Matapishi njiani wala sina hamu
Jamaani
Tuache jamaani
Tunza usafi kuanzia kwako nyumbani
Vibarazani na pia hata njiani
Tujitahidi jamani Zanzibar yetu ni shani
Tumejaliwa wageni, tunza zidi kungari
Kwerekwe, Forodhani
Michenzani, Darajani
Pendezesha jiji kama sifa ya dini
Jirani
Sidharau jirani
Jamaani
Tuache jamaani
Basi tupa kwenye bin
Tapika kwenye bin
Nidhafu ndio maadili
Usafi ndio deen
Basi tupa kwenye bin
Tapika kwenye bin
Nidhafu ndio maadil
Usafi ndio deen
Tupa kwenye bin
Weka kwenye bin
Nidhafu ndo maadil
Usafi ndio deen
Tupa kwenye bin
Weka kwenye bin
Nidhafu ndo maadil
Usafi ndio deen
Usafi ndio deen
Usafi ndio deen
Aah Mzanzibar
Inuka
Saidia
Mazingira
Aah Wazanzibar
Inuka
Saidia
Mazingira