Tausi ft. Mbosso Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2022
Lyrics
Tausi ft. Mbosso - Mrisho Mpoto
...
mocko
Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako
Karibu Tausi
karibu Sana Tausi
mchezo uliotukuta nao ni wasandakalawe Amina mwenye kupata kapata mwenye kukosa akose
Kipapatio Cha kuku ugali mweusi
Analiaje kwiu kwiu
Mpaka Lin mwenye kupata apate
mpaka Lin mwenye kukosa akose
Asante Tausi
Umeukataa mlio wa kwiu kwiu
Na rangi ya kuku kugawana
Tausi
Harufu unayoisikia ni yachakula walicho kula
Wameamua tu kujisaidia nyuma ya nyumba ili harufu irudi ndani kumchefua mpishi
Usishtuke ndivyo ilivyo kwa watu wenye shibe
Tausi
tumbo lenye kukataa huleta tu mawe mawe
Unapo taka kuwatambulisha watoto wako kwa wageni tumia idadi yetu na sio majina
Maana baadhi ya wanao wanatumia A.K.A siku hizi watakuvuruga
kumbuka vita la kumbi ni fungate lililo fungwa kwa mkazo halipaswi kumuumiza mbebaji
Karibu Tausi
Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako
Tausi Mimi mwanao baada ya kutoka jandoni
Nilidhani mm ni mkubwa sasa
Naambiwa ooooh hicho kilicho tolewa ni kipande Cha ngozi tu
Hakina mahusiano na kukua kwako
kwel inamaana Kila anaye ingiza kidole puani anamashaka na alicho nusa
Uliwahi kusema wewe mwenyewe
Mnyonge hapigani kwa fedha
Na tulifanya makosa kuchagua silaha
Silaha tuliyo ichagua itatutia unyonge
Na kuondoa unyonge kwa kutumia silaha za wenye nguvu ambazo sisi hatuna unazid kupoteza muda
Muda upi wasisi kukua au nyakati
Tausi nimeamini asiyeona anapotumia torch sio kwaajili yake anawamuoikia wanao ona ili wasimkanyage
na ili iyote Tausi lazima ioze Kila mwenye zamu yake asiache kumwagilia
aaaahaaaaaahaaahaaaaa
viriboto kupe huretaga virusi Tausi
ukuta mweupe wausiufanye mweusi Tausi
Tausi wewe
Tausi wetu
Karibu Tausi uipambe nyumba yetu
Tausi wewe
Tausi wetu
Mpendwa tausi mwayangu mwana kwetu
Chanua mbawa zako Tausi
Waione rangi yako Tausi
Mpole sauti hiyo ndio sifa yako Tausi
Chanua mbawa zako Tausi
waione rangi yako Tausi
Jichunge Tausi
wasinyofoe nyoya lako
added by
Prince wa kigoma
Mocko genius