Nimwage Radhi Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2021
Lyrics
Nimwage Radhi - Mrisho Mpoto
...
Instruments
Alili liliii
Furaha isiyo kifani
Kumpata mwandani
hakika wamependeza
goma lipo uwanjani
kaibiwa nani
sa unaachaje kucheza...!
Ama kweli harusi imefana tena ya kihistoria
pande zote! baba na mama naona wanashangilia
ila sitaki kuwa mnafiki jumba bovu kuniangukia
nina langu la moyoni
ningependa kuwaambia
Bi harusi mashoga wa kupupia hao ni wa kuwangalia
wako wale wa hali gahn...wanakuja kuchungulia uwaombe samahani uwakomeshe wambea,
eti wifi umepika nini na mimi utanigaia?
waambie wapika dagaa wenye pilipili nyingi zinakutosha wew na mume wako,
wako wao watakimbia.
Eeeh....!
Aiiih shemeji chukua ya mumeo
usiskize ya fulani
Na hii ndio meseji sema na mumeo usifuate ya jirani
kwa furaha niliyo nayo niacheni nimwage radhi
alilililiiiih,
mi nataka nimwage radhi,
Aiyoyo niacheni nimwage radhi
mi nataka nimwage radhi! alilililiiiih
Ng'ombe anapoita ndama tunasema kuwa analia,
kupigwa na kulalama hatujawahi kuskia
hakika mmependeza
ninavyomfahamu bi harusi sipati kusimulia
nimetokea ruvuma,mchomoro namtumbo lindi mtwara mpaka chitohori nimezisikia
sifa za binti huyu molaa amemjalia
binti hapendi majungu hakika nachowaambia ukimuazima viatu na gauni anakuachia
Bwana harusi tunakupa mke ukaishi naye vyema nyumbani
huna kitu usimfiche mwambie taabani
ikiwezekana mkakope mkono uende kinywani
usimpige mateke
kisingizio kitu fulani
oooh umefanya nini jana hakuliki leo ndani
mtoto bado mteke usimkomaze kwa ngumi
ukimshindwa mrudishe kwao hajaua huyu
Mumeo akienda kazini
akirudi salimia
wala usikae chini chakula kumsukumia
mkaribishe ndani hali ukimjulia
muulize za kazini kwa tabasam murua
kisha msindikize bafuni hata kama anapajua
Alafu wew tafuta kiti jikoni kimbilia
Chukua simu yako meseji ukimtumia
mwambie
Asilani bila wewe chakula hakitaingia
Eeeh....!
Aiiih shemeji chukua ya mumeo,
usiskize ya fulani,
na hii ndio meseji
sema na mumeo usifuate ya jirani
kwa furaha niliyo nayo
Niacheni nimwage radhi
alilililiiiih
mi nataka nimwage radhi,
Aiyoyo niacheni nimwage radhi,
mi nataka nimwage radhi!
alilililiiiih
Nawaomba niishie hapa
taharishi huwa hafungwi
Naomba nichape lapa
yaliyobaki ni ya makungwi
niliowakera samahani
kusema ni jukumu langu
nawaomba muishe kwa amani
hiyo ni furaha yangu
mmmmh
ndoa ni kama safari
tuombe yake dua
atuepushe na shari
saa chini ya jua
Ah somo yake mwali
Ainuke
Mama yake mwali
Ainuke
Baba yake mwali
Ainuke
Aje kati tulicheze goma
Ah mama yake mwali
Ainuke
Dada yake mwali
Ainuke
Shangazi yake mwali
Ainuke
Aje kati tulicheze goma
Niacheni Nimwage radhi
Mi nataka tumwage radhi
Niacheni Nimwage radhi
Mi nataka tumwage radhi
lyrics by NjauMsafiri