Amani Lyrics
- Genre:Pop
- Year of Release:2021
Lyrics
Amani - Wanavokali
...
Hawaoni kuwa
Kidole kimoja hakiwezi kuvunja chawa
Bila ya kujua
Kufanya kazi na wenzio kwa pamoja
Tutajiinua
Na mambo yote yatarudi kuwa sawa sawa
Na tunapiga dua
Kwake Mwenyezi atuelekeze tukikosa njia
Na matumaini yetu yote yakianza didimia
Hatatuwacha kwenye njaa na mwishowe tutapaa
Amani
Amani iwe na wewe
Na uzuri
Uzuri wako usipotee usipoteze
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe
Nataka niwe mwepesi wa rohoni
Saa zingine macho tu hayaoni
Hivo niweke kwenye maombi
Ndoto zisibaki ndotoni
Nitakapotoka gizani (gizani)
Na nitakaporudi nyumbani
Atanipanguza machozi
Sitolia kama awali
Napiga dua
Kwake Mwenyezi atuelekeze
Tukikosa njia
Na matumaini yetu yote yakianza didimia
Hatatuwacha kwenye njaa
Na mwishowe tutapaa
Amani
Amani iwe na wewe
Na uzuri
Uzuri wako usipotee usipoteze
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe, Amani iwe na wewe
Amani iwe nawe