Ayubu ft. Eric Kisindja Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2019
Lyrics
Ayubu ft. Eric Kisindja - Natasha Lisimo
...
Ayubu wewe wawezaje kuwa bubu
Si hauna haja ya kusifu
kufuru Mungu wako na ufe
Lakini simwabudu kwa alichofanya
Na wala si kwa wingi wa vitu
Bali ni kwa jinsi alivyo
Ayubu! wewe hauna afya
Umepoteza mali, Watoto, marafiki
U t a f a n y a nini!?
Mimi nitamuabudu
Hakika nitamuabudu
Mimi nitamuabudu
Aliniumba ili nimwabudu
Bwana amenipa na Bwana ametwaa
Jina la Bwana na libarikiwe
Nita nitamsifu na kumsifu
Heeeee, Je wewe
Utashikamana na ukamilifu wako!?
Mkufuru huyo Mungu wako
Ayubu na ufe
Wanena kama mwanamke mpumbavu
Je tupate mema mkononi mwa Mungu
Na tusipate mbaya!?
Ayubu wewe huna Afya,
Mwili mzima umejaa majipu na madonda
U t a f a n y a n i n i?
Mimi nitamuabudu
Hakika nitamuabudu
Mimi nitamuabudu
Aliniumba ili nimwabudu
Bwana amenipa na Bwana ametwaa
Jina la Bwana na libarikiwe
Nita-nitamsifu na kumsifu
Hata kama unapitia changamoto yoyote
Usikufuru na kumwacha huyu Yesu wako
Tumeona mwisho wa Ayubu
Bwana akamrejeshea
Bwana amerejesha
(Watoto, Mali)
Mara mbili karudisha
(Hajawahi shidwa Yesu)
Bwana amerejesha
(Watoto, mali, upendo)
Mara mbili karudisha
(Upendo hupatikana kwako Bwana Yesu)
Bwana amerejesha
(amenirejeshea heshima)
Mara mbili karudisha
(Nani Tena)
Bwana amerejesha
(kuinua mfalme)
Mara mbili karudisha