![Nimenogewa ft. Bando](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/11/15/f8d7dcca45cf4050b33a2b97143f1c9fH3000W3000_464_464.jpg)
Nimenogewa ft. Bando Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2024
Lyrics
Nimenogewa ft. Bando - SheIsSiena
...
(we mkaka.....)
Verse 01
Siena
Mwenzenu nimeshikwa na huba
moyo wangu huyu mtu kauiba
Na niseme kweli ameweza kunificha
kwenye lake pori la mapenzi sitotoka
Hili penzi la Runingo nishakata kwako nakuzingo
Nitafanya kila kitu kukulinda, Nipe chuzi nikupe Dundo (we kaka we..)
Bridge.
Dj weka Music mi ninataka cheza..
kwenye hili letu Penzi mi ameniweza..
Mmh..
kama ni raha basi zinaboa
Nadezwa ye ananikomoa
Alivo fundi ye ananipatia
Hakuna kitu hajanifanyia
Nikiwa naye ninajiachia
Ni siri gani mi hajanambia (haipo..)
Chorus.
Nimenogewa kua naye
Penzi lake lanifanya nipagawe
Nimenogewa kua naye
Penzi lake lanifanya nipagawe
Instumental..
Verse 02.
Bando
Eeh.. nashida ziliondoa watu nawahitaji
Wengi waliniacha wakaenda
hapo ndo nilijua wazi yupi anayenipenda
Na yupi wa starehe hata ikipita miaka kenda
Asante kwa kunauza Tarehe ili ununue kalenda
Aa.. Mapenzi yananjia mbili kuu
Hizi alisema babu kijijini nanukuu
Mapenzi ni mualiko usio na kadi maibuu
Kama mapenzi ni ugonjwa naomba nisipate nafuu
Uko fiti na mapenzi ya dhati umebobea
Upendo kama mchicha shambani jua unajongea
Na wakiongea naomba wapaliwe mpaka chafya
Wakisema nakuchezea waambie mapenzi ni afya
Bridge
Dj weka Music mi ninataka cheza..
kwenye hili letu Penzi mi ameniweza..
Mmh..
kama ni raha basi zinaboa
Nadezwa ye ananikomoa
Alivo fundi ye ananipatia
Hakuna kitu hajanifanyia
Nikiwa naye ninajiachia
Ni siri gani mi hajanambia (haipo..)
Chorus
Nimenogewa kua naye
Penzi lake lanifanya nipagawe
Nimenogewa kua naye
Penzi lake lanifanya nipagawe
Instrumental..
lyrics by
@jacktons86