Kama ni Kwangu Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2024
Lyrics
Hazina za jana niliacha kuombea
Matakwa ya kesho nikikosa sitalia
Tayarisha nyayo leo mi ninatembea
Imarisha wazo lisemalo endelea
Mi siangalii nyuma tena
Sina adui nyi nyote napenda
Njia ya roho siezi poteza
Nguvu za kubuni ninaongeza
Watu kunipinga mimi sitahofia
Wengi watafuta nia watakufia
Kwa vita we jua kuna wenye faida
Kwa konde na pana uovu hauwezi shinda
So tell me what you want from life
Ukikata tamaa are you really alive
Wengi wetu pesa, wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
So come on tell me what you really want from life
Ukikata tamaa are you really alive
Wengi wetu pesa, wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
Kama ni kwangu
Mambo ya ulimwengu ni mengi sana
Sayari kwa Mungu labda ni Sanaa
Akili yangu mara nyingi hupenda kupaa
Kupenda kwangu ujuzi siezi ogopa
Kawaida yetu kubaki tunapojua
Ni jukumu letu maisha kufafanua
Kuelimishana hekima huwezi ficha
Bado twabishana wana wetu piga picha
Kiwewe kuenea, hatuwezi endelea
Niaje tutapona riziki twapigania?
Pesa bila thamani tukijipata jangwani
Ukweli tunajua, wa kutumia ni nani?
Mali ya ukweli we jua haiozi
Mali ya ukweli haishikiki na mwizi
Mali ya ukweli endeleza tamaduni
So, come on, tell me what you really want from life
Ukikata tamaa, are you really alive?
Wengi wetu pesa wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
So, come on, tell me what you really want from life
Ukikata tamaa, are you really alive?
Wengi wetu pesa wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
Kama ni Kwangu
Wasema kila mtu alizaliwa na nyota
Kivuli cha usiku kikija ndoto twafuata
Kizazi kipya tuwasili imani hawawezi pora
Nguvu ya kweli akili angani nje ya kiota
Naam, dada, naam, kaka
Wakati wetu umefika
Waamini hautaweza
Nashangaa ni nani alikwambia
Kitu chenye naombea ni wimbo kuhamasisha
Shauku rohoni utu kweli kuamsha
Hatima karibu wewe skiza ikibisha
So, come on, tell me what you really want from life
Ukikata tamaa, are you really alive?
Wengi wetu pesa wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
So, come on, tell me what you really want from life
Ukikata tamaa, are you really alive?
Wengi wetu pesa wengine ni uhuru
Evolution, elevation kama ni kwangu
Kama ni Kwangu