
Glory ft. Gifted Lyrics
- Genre:Classical
- Year of Release:2024
This song is not currently available in your region.
Lyrics
Glory ft. Gifted - Fid Q
...
Hhhhhhhhh!
Glory!
Hhhhhhhhh!
Glory!
Hhh! Hhh! Hhh! Hhh! Hhh!
Glory!
Hhh! Hhh! Hhh! Hhh! Hhh!
Glory!
Hhh! Hhh! Hhh! Hhh! Hhh!
Glory!
Nilikua kama dira, sina kazi baada ya chombo kutia nanga, au kama tiba.
Sikua na mchongo baada ya mgonjwa kukata kamba, mshumaa uliozimwa baada ya macho yao kutanda. Sujaa alieamini wenye vyeo hawawezi tamba, nilitupwa kama pingu ya mfungwa alietoka jela, au fimbo ya kipofu baada ya mpofu kuiona hela. Hamkuona mzazi baada ya mtoto kujua kutembea, nilisuswa kama boya mbele ya wajuaji wa kuogelea. Nilishindwa kila vita nilipigika kama mjinga, sikuwahi kuamini, kuna siku na mimi wataniita bingwa. Wenzangu wakaanza kuwalipa, mbona kwangu miamala haisomi, nikaumiza kichwa ili mipango isigome, wakiweka milima mimi naigeuza vitonga. Hata nusu ya hatua ni hatua, mdogo mdogo nikawa nasonga, japo mwendo wa kinyonga. Mbegu ili ichepue lazima ioze kwanza mjomba. Mtaani nakuta wana wananisema sema siwezi, ndani yangu nasikia sauti inaniambia jamaa unaweza. ANGUKO lina herufi sita, MWAMKO linazo pia, HUZUNI lina herufi sita, FURAHA inazo pia.
Mmh! Utukufu ni wako baba, (unako) sifa zote unastahili (sifa zote ni zako) sio leo tu hata jana umeonesha unanipenda mimi.
Mmmmmh!
Hhh! Hhh! Hhh! Hhh! Hhh!
Glory!
Hhh! Hhh! Hhh! Hhh! Hhh!
Mmmmmh!
Glory!
Nilijihisi kama, koroboi lilozimwa mida ya machweo,fukufuku lilotoswa kiwavi hakigeuki kipepeo. Mswahili alokwisha baada ya elimu kupatikana, sikujua mapito n'lopita n'kipimo cha uungwana. N'liachwa kama kiota ndege alipojua kupaa, mateso hayakua ajali bali ni mzani wa ushujaa. N'likua nanuka, haukuona kinyaa, ulin'nyanyua n'kanyanyuka sa kila kona nang'aa. Nloyapitia yalionyesha nguvu n'lonayo, majaribu yakauibua ujasiri n'liopewa na mayo. Nikawa hodari n'kaeza kuukabili utata, ndoto n'lokua nayo imegeuka uhalisia safi. Umefanya nijiamini pasi na kuweka chembe ya uwoga, nimekubali nilihitaji nianguke, ili n'nyanyuke nikiwa ngangari. Usikate tamaa au kuhofia, KUJIKATAA ina herufi tisa, KUJIAMINI inazo pia.
Utukufu ni wako baba, (unako) sifa zote unastahili (sifa zote ni zako) sio leo tu hata jana, umeonesha unanipenda mimi.
Utukufu ni wako baba, sifa zote unastahili, sio leo tu hata jana, umeonesha unanipenda mimi.
Glo! Glo! Glo! Glo! Glo! Glory!