Nisubirishe Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Muumba mbingu muumba dunia, Visiwa vya pwani
Muumba bara na vilivyomo
Dua zangu wazisikia nikisalisali
Ndivyo neno lavyoniambia, Naamini
Ila mbona, nahisi uko mbali nani?
Mbona wakati wangu haufiki
Hatua moja mbele, narudi na mbili nyuma ah
Kwani niko pale pale
Ile ile shaka ya moyo wangu
Niondolee nikuamini we.
Niondolee shaka moyoni mwangu, nikuamini
Niondolee pupa moyoni mwangu, nisubirishe
Naamini wafahau ninachopitia, siko shwarishwari
Mambo yangu yanazamia
Kwa huduma nimejitolea, naokoa jahazi kutangaza wewe ni donor
Siamini
Mbona nahisi uko mbali nani
Mbona muujiza wangu haufiki
Moyoni natamani nisubiri kusudi lako
Ila unyonge mwilini ni ule ule
Wewe ndiwe, amani ya moyo wangu
Niwezeshe nikuamini we.
Niondolee shaka moyoni mwangu, nikuamini
Niondolee pupa moyoni mwangu, nisubirishe
Eloi eloi lamasabakithani
Baba mbona umeniacha
Niondolee shaka moyoni mwangu, nikuamini
Niondolee pupa moyoni mwangu, nisubirishe