Amani ya Mungu Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Penye joto jangwani hakuna kivuli
Maisha yenye kiu njaa na wasiwasi
Ndipo mto mzuri unatiririka
Waongezeka kina pia upana wake
Kwa utulivu mwingi lakini kwa nguvu kuu
Kwa sauti tulivu maji yanatembea
Kwa sauti tulivu na kwa uhakika
Amani ya mungu kama mto hushinda yote
Kumjua sana huyu mungu huleta nguvu
Mema mengi yapo mbele yetu yatungojea.
Hutunyeshea mvua kiu yatulizwa
Maji hutiririka twaridhika mioyo
Kwenye viganja vyake Bwana
Hutulaza twapata Amani
Amani ya Mungu (bwana) ni zawadi kwetu
Tunapo muamini hutupatia twashinda yote
Amani ya mungu itujaze mioyoni mwetu
Amani ya Mungu itujazee ituongozee
Tushinde Yote