Nena Bwana Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Nena Bwana - Anointed Singers Tz
...
Nena Bwana ndani yangu
Nena ninasikiaub
Sauti yako nataka
Niisikie sasa
Ukinena unaponya
Pia unabariki
Ukinena waokoa
Nena twakusikia
Nipo tayari Bwana
Kusikia unenapo
Nina shauku kubwa
Kukusikia Bwana
Sauti za dunia
Zanipotosha pabaya
Sauti yako pekee
Nataka kusikia
Twaweza kuisikia
Sauti yake Mungu
Kupitia Neno lake
Maombi na Ibada
Hivyo na tuwe tayari
Kumsikia Mungu
Anaponena na sisi
Tuweze kumsikia
Nipo tayari Bwana
Kusikia unenapo
Nina shauku kubwa
Kukusikia Bwana
Sauti za dunia
Zanipotosha pabaya
Sauti yako pekee
Nataka kusikia
Nipo tayari Bwana
Kusikia unenapo
Nina shauku kubwa
Kukusikia Bwana
Sauti za dunia
Zanipotosha pabaya
Sauti yako pekee
Nataka kusikia
Nataka kusikia...