Upendo wa Mwokozi Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Upendo wake Mungu ni mkuu
Hakuna lugha ya kuueleza
Wala hakuna cha kulinganisha
Na upendo wake juu yetu
Aliicha enzi yake juu akashuka niokoke
Siwezi kuueleza upendo wa Mwokozi
Hakuna giza kuu ambalo
Mwanga wa upendo wake hautapenya
Hakuna moyo ulio mgumu asioweza kulainisha
Aliicha enzi yake juu akashuka niokoke
Siwezi kuueleza upendo wa Mwokozi
Upendo wa ajabu kumtoa mwana wake