
Shuka Zakayo Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2019
Lyrics
Shuka Zakayo - Kisumu Central AYM
...
Safari ya Yesu kutoka Yeriko,
Akiwa bado njiani,
Alimwona Zakayo mtu mfupi,
Akiwa juu ya mkuyu,
Akamwamuru Zakayo ashuke,
Waandamane nyumbani,
Shuka,Shuka(Shuka) Zakayo,
Leo mi ni mgeni wako.
Tujinyenyekeze mbele ya Yesu,
Tatusamehe na kutupokea,
Kama Zakayo alivyojishusha,
Nasi tuige,
Mfano huo,
Tupige hatua ya imani,
Mwokozi atatuweka huru.
Mtoza ushuru,
Mfupi wa kimo,
Lakini ni wa imani,
Alimkaribisha mwokozi nyumbani,
Nakula pamoja naye,
Karudishia watu mali zao,
Kwa kuwalipa mara nne,
Na mara hio huyu Zakayo,
Kabadilika kawa mpya.
Tujinyenyekeze mbele ya Yesu,
Tatusamehe na kutupokea,
Kama Zakayo alivyojishusha,
Nasi tuige,
Mfano huo,
Tupige hatua ya imani,
Mwokozi atatuweka huru.