
Sala Yangu Na Ipae Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Sala Yangu Na Ipae - Rajo Productions
...
Sala yangu ipae mbele yako Bwana * 2
{ Kama moshi wa ubani altareni,
Na kuinuliwa kwa mikono yangu
Iwe kama sadaka, sadaka ya jioni } * 2
Ee Bwana tunakutolea sadaka yetu,
Pamoja na maisha ya kila siku.
Uwe radhi kuipokea sadaka yetu,
Kama zile za mababu wa zamani.
Hivyo sadaka ifane mbele zako Bwana,
Na iwe sadaka ya shukrani kubwa.
Nasi utubariki maisha yetu yote,
Na mwisho utujalie heri yako.