
HAWAJUI Lyrics
- Genre:Spoken Word
- Year of Release:2023
Lyrics
Tulipofika ni mbali
Itisha madafu utulize akili
Keti chini nikusimulie hadithi za Misambwa
Na Masinde wa Nameme ohkwa Mwasame
Godpapa wa dini ya Musambwa
Babu aliniambia alikuwa msumbufu kweli
Sijui kama walijuana
Lakini najua alileta shida sana hata baada ya kifo
Kabla ya kuaga, unajua alifanya nini?
Sikiza
Aliagiza mti wa mkuyu utolewe na mizizi yake
Ili kuipa njia kaburi lake
Familia nayo iliamua kupuuzia mbali na kumzika kwingine
Lakini
Shaka
Walipata kaburi la mtu mwengine
Katika ile sehemu waliyojichagulia wenyewe
Mwishowe alizikwa kama alivyoagiza mwanzoni
Anyway, alikuulizia mama
Najua anakuenzi
Nilimwelezea unavyoipa pumzi yangu maana
Ninavyokupenda zaidi ya mapenzi na mapeni
Nilimwambia asianze haraka za harusi au wajukuu
Najua tayari keshaanza kutenga visenti vya kuku na zawadi za leso
Tukifika kule vumilia
Usidanganywe na tabasamu za majirani
Watakumeza mzima mzima
Salamu ziwe za hewani kama za Corona
Waambie unaumwa na tumbo so huwezi kula chochote
Najua tunatofautiana kimila na safari hii si ya wengi
Yamesemwa mengi sana juu yako na wenye akili ndogo lakini usi-mind
Those are just stereotypes that entertain narrow minds
I'd fall for the hills of Murang'a again if I had to do it nine thousand times
A thousand for each daughter of Mumbi
Tafadhali wavumilie mama na baba
They grew up under those dividing myths lakini
Wanajitahidi kukuchukua kama binti yao
Ipe muda
Dada zangu wakiongea kwa lugha ya mama usichukulie vibaya
Haupo kwenye maongezi yao
Najua kidogo itawauma kujua kaka yao wa kipekee
Karibuni atakuwa na familia mpya
Lakini niamini
Wewe ni familia yao pia
Usiskize ya watu
Barabara tulizopitia hawazifahamu
They don't know what it took for us to smile
They didn't see us crawling to this place
Hawakuona machozi yetu juu walikuwa busy na rangi ya lipstick kwa mdomo
Na eyebrows zilivyochongwa
Tukimeza bitter saliva walidhani ni utamu wa maisha tuna-sample
Hawakuona ilivyokuwa ngumu ku-swallow
Walituandalia meza wakasahau viti ndiyo watukalie
Si unajua binadamu ana roho ngumu
Yasikutishie hayo
Nipe mkono wako
Nitakuwa shujaa wako
Nitakufariji
Nitakulinda
Wacha upinde wa mvua na furaha ukumbatie moyo wako
Jua lichore tabasamu usoni na mawingu ya uwoga yapotee
Safari ya mbali huanza na hatua na mbugani ushatua
Jihisi nyumbani ukiwa nami