
HEAVEN'S CRY Lyrics
- Genre:Spoken Word
- Year of Release:2023
Lyrics
Uli-rest in peace ukaniwacha niki-live in pieces
Maneno si enough kuziba crevices
Cracks zimejaa kwa roho sijui nini itafunika
Hizo pieces zilibaki sijui nani atashikanisha
Napagawa na machungu bila wa kunitibu
Nimejawa maswali kuliko majibu
And to be honest
I've been trying to avoid this talk
Ladha ya mtandao ilinitoka hiyo siku
They said not to shoot the messenger
But risasi yangu ni Twitter ilipokea
I wish ningeweza cage hiyo blue bird niitupe baharani
Maybe the oceans would carry it along with my pain
Maybe the waves would kill this lump in my chest
Maybe the water would drown my sorrows and put me to rest
Maybe we wouldn't need to have this one-sided conversation in the first place
Maybe
Siku ya kulipa respects za mwisho nilishindwa kuja
Na hiyo deni sioni nikilipa
I forced myself to forget the day it happened
I didn't want the calendar to take me back to that moment every single year
Wacha last memories ziwe za hiyo bedsitter
Tukisikiza ngoma za Pompi na Mag44
Conversations za ku-make it na Poetry na njama za kuomoka
Plans za ku-market kazi ya Qui ivuke borders
Mo akiitisha sweater juu ya baridi sisi tukimcheka
Cracking jokes tukihesabu chupa za soda chini ya sink
Celebrating the little steps za my folks in regaining her memory
By the way, zile prayers tuli-make zilianza kujibiwa
Kamiti YCTC angalau wanashughulikiwa
EP na kitabu nimewachilia
Ndoto zetu sasa zinatimizwa
Kuna mengi tulipanga but life ikatupanga
Kifo ikapangua
Siwezi sema niko sawa
Bado saliva ni sour
Ina-feel kama acid kwa throat
They talk a lot about what the reaper takes
But it's not what it takes from us
But what it leaves behind
Memories
Laughter
Warmth
To haunt the living to death
Questions that I have no answers to
Uli-feel pain kweli?
Hiyo text ilikuwa utume ilienda?
Ulijua itakuwa hiyo siku?
Thoughts gani ulifikiria za mwisho?
Malaika walikukaribisha?
Niambie majibu nitapata lini
Juu Mo bado anakungoja
Anajikaza kila siku lakini hata kamba imekazwa sana hulemewa
Inaumiza sana kuona nguvu yake ikikatika
Sijui nimwambie maneno gani kumpa comfort
Sijui nifanye nini asi-drown na mawazo
Nitumie sign angalau
Unamjua zaidi ya sisi
Nifanye nini aweze ku-smile?
Nimpeleke wapi a-feel alive?
Nimpe nini a-feel anapendwa?
Nitamwonyeshaje bado unampenda?
Naogopa kuambia Kena about you niki-speak in past tense
Akianza kukuulizia sijui nitaangalia wapi
Bado uko kwa roho na akili yangu
Kwa mawazo bado naku-feel
Sijui nitangoja hadi lini
How long will I feel this empty?
I don't know
Cause I'm not ready to let you go