
MPITA NJIA ft. SLB & Emma Ndire Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2022
Lyrics
Skiza unachoambiwa
Skiza mama, baba, ndugu, wale wadogo pia
Skiza wale wazee, hadithi watakusimulia
Skiza anayekufunza, anayekupikia
Mungu yu kwa mpita njia
Usidhani utaweza, bila kuteleza
Pahali unaenda, bila kuelekezwa
Hiyo njia unayopitia, mimi nishashuhudia
Ni miaka zimenipita, si kwamba nimesahaulika
Sisi ni wale watu, wale watu wazima
(Na) Mamlaka tunayo kupita mipaka Africa
Usiwachane naye, pita pale naye
Mweke karibu, usiende mbali naye
Choma nyama naye, piga bia naye
Lakini mwishowe, panga maisha yako na yeye
Skiza unachoambiwa
Skiza mama, baba, ndugu, wale wadogo pia
Skiza wale wazee, hadithi watakusimulia
Skiza anayekufunza, anayekupikia
Mungu yu kwa mpita njia
Hii story iko ngori, twende kazi
Vila milima tulipima tukitafuta maji
Tulienda bila gari, tukihata hizo risasi
Huku kwetu hakuna miti kumejaa nyasi
Sisi ni wale watu wale watu wakubwa
(Na) Ukienda hapa, pale, kule wanatutambua
Usiwachane naye, pita pale naye
Mweke karibu, usiende mbali naye
Choma nyama naye, piga bia naye
Lakini mwishowe, panga maisha yako na yeye
Skiza unachoambiwa
Skiza mama, baba, ndugu, wale wadogo pia
Skiza wale wazee, hadithi watakusimulia
Skiza anayekufunza, anayekupikia
Mungu yu kwa mpita njia