
Karibu Na wewe Lyrics
- Genre:Soul
- Year of Release:2017
Lyrics
Karibu Na wewe - Nuru Kitambo
...
Karibu na wewe,
Mungu wangu
Karibu zaidi,
Bwana wangu
Siku zote niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.
(Instrumental)
Mimi nasafiri
Duniani,
Pa kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.
(Instrumental)
Na kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba, uwe maji
Ya wokovu;
Mashakani niwe
Karibu na wewe;
Karibu zaidi
Mungu wangu.
(Instrumental)
Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu,
Zikikoma hapa
Siku zangu,
Kwa furaha niwe
Pamoja na wewe,
Karibu kabisa
Mungu wangu.