
Maombi Asikia Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Maombi Asikia - Miriam Thomas Chirwa
...
nasema nawewe uliyekata tamaa
kila kitu kwako unaona huwezi
Yesu aitapo upendo wake
ataka uje kwake leo
Hakuna mwingine mwema
wa kutuhurumia
atujua tu dhaifu
dua atasikia
rafiki uliyedharauliwa
huoni mwingine wa kukutia moyo
ila Yesu wa msalaba yupo kwa ajili yako
kwa ombi akusikia
Hakuna mwingine mwema
wa kutuhurumia
atujua tu dhaifu
dua atasikia
usihofu kila unayoyapitia
maana Mungu ataka wewe uwe hodari
ataka wewe usimame uwe karibu nayeye
ukishindwa muite yeye
maana hakuna mwingine mwema
wa kutuhurumia
atujua tu dhaifu
dua atasikia
kuna watu wengine ni marafiki zetu
hatuwapi moyo ila kuwavunja moyo
ila Yesu rafiki aliye mwema
atatushangaza maana anawapenda
Hakuna mwingine mwema
wa kutuhurumia
atujua tu dhaifu
dua atasikia