We Ndo Mchizi Wangu RMX Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2019
Lyrics
We Ndo Mchizi Wangu RMX - Nako 2 Nako
...
[FID Q]
Fiddy Q hili jina tu lina ring bell
kimziki niko juu vina vinabring sense
mi mi mi ndo mchizi wako
we we we ndo mchizi wangu
natamani steve 2k angekuwepo
ye ndo mchizi wangu kama pingu na deso
majaribu ya leo sio majibu ya kesho
nisipende sana kukaza ingawa nauza ka' commercial
aliniambia mengi ya kuchunga
kama begi la abiria kwenye stendi afungwa
mchizi sikusoma naye tulikutana tu mtaani udogoni
skucheza naye ye ndo mchizi wangu wa ukubwani
hakufurahi nilipoanguka alipenda nikamate line
sasa inabidi wanibanie ili Maemcee wengine wa'shine
[CHIDI BENZ]
chidi go, chidi so, chidi ndo king wa ku'flow
chidi style, chidi mathematical nawakaba koo
chidi king, chidi ana'shine bila hata bling
chidi cool, chidi full, chidi so fresh so clean
sipimiki mwenye crown ya freestyle
nawaacha mbali kama forty five thou miles
we we we ndo mchizi wangu
nipe tano ngum ngum! changu changu chako changu
One love kama chidi na Nako
kama mdogo na macho
kama kiuno na tako
kama pop na rako
kifo na roho yako
popote unionapo
mi ndo mchizi wako
mtoto wa ilala, mwenye love na mabinti
love na ma niggaz
love love kwa street
mi sio mkali zaidi ya
mi ni mkali zaidi yao
na ndo maana ushindi wangu
mi
[GEEZ MABOVU]
unayejali utu na sio hizo thumni
mwavuli kwenye mvua
kivuli kwenye jua
sina cha kukulipa zaidi ya njema dua
sometimes mitikasi inafanya hatuonani
lakini usihofu siwezi poteza imani
moyoni we ndo mchizi
sio leo tangu zamani
na huu ni waraka wako basi nisome hewani
if i die before i wake you should know you're my best
dont cry cause of my death [what to do?] cover my place
rithi kilicho changu jali huu utamaduni, ah temba
we ndo mchizi kati ya hawa kumi
[TEMBA]
eka uzito kwa mwanangu nipe gwara mchizi wangu
ili taifa tulijenge tusilitupe jembe, na ukifa kwa kiu baharini huo ni uzembe
mi nna wivu wa maendeleo na upeo kila leo
ndo maana machizi wangu temeke wananipa vyeo
wanasema naweza kizazi changu nakieneza
na ulita kilegeza mimi nammeza
okay sikiliza pusha kama una njaa rusha
kama tulivyozungusha
kizuri kula na ndugu yako na usisahau masela wako
mtembea bure si sawa na mkaa bure
hakuna ujanja zaidi ya shule muulize hata sule
ni mchizi wangu kitambo alishakwendaga ng'ambo
sasa karudi anafanya mambo ah
we we we ndo mchizi wangu
we we we ndo mchizi wangu, ah yeah
[MWANA FA]
moyo unanienda mbio kama unaendeshwa na schumacher
kila nikiwaza mchizi wangu huenda unateseka
kwangu ni zaidi ya pacha binamu wa haswa haswa
siwezi kuacha ukichoreka siwezi kuona unanyanyaswa
mi ni kivuli chako siwezi kuacha kukufuata
na kufeel ile kinoma zaidi ya maelezo si mzuka?
i dont deserve you najua we nakuona kama zali
we kwangu zaidi ya zawadi imeoshwa na mchanga wa kaburi?
naiendesha DSM so wanachonga sometimes
zibia masikio vitu vibaya ndo walivyo wanadamu
nawachukia kama askari wa jiji
achana na wachimba chumvi wananiamsha usingizini wanipe dawa ya usingizi?
nakuombea mazuri cause we ndo mchizi wangu
ill catch your back siku zote hesabu kwa hilo mwanangu
we we we ndo mchizi wangu
we we we ndo mchizi wangu, yeah
we we ndo mchizi wangu
usinihukumu kutokana na dhambi zangu
ili urafiki udumu tuwekane sawa mwanangu
ah, amini kwamba shida yako shida yangu
kama una ladha kweli basi we ndo mchizi wangu
kitaani hatuelewani ma'snitch sio wanangu
nasamehe mara sabini sina bifu moyoni mwangu
naishi nitakavyo mimi na simuigi mwenzangu
wapo ma'fans wangu wapo maadui zangu
wapo ma'snitch wangu, we ndo mchizi wangu
we ndo mchizi wangu
mtoto wa kitaa what?