Hujanizidi ft. D Voice Lyrics
- Genre:Bongo Flava
- Year of Release:2024
Lyrics
Hujanizidi ft. D Voice - Zuchu
...
INTRO
Ah-yah-aya, ah-yah-aya, oh, ah-yah-aya
(Diblo One Touch)
VERSE
Yaani mara kumi ungekuwa mbaya, halafu ungekuwa na hela
Lakini tatizo lako mbaya halafu hauna hela
Ni mara kumi ungekuwa kijuso, halafu ungekuwa na hela
Ila tatizo lako kijuso halafu hauna hela
PRE-CHORUS
Ah, sa' mbona unapata tabu kujichubua
Tako huna unaforce kujibinua
Baby wangu hajadata na chura ka' hujajua
Kadata na mambo matamu ninayomgea, nikwambie wewe
CHORUS
Kwa uzuri hujanizidi mimi
Kwa utamu hujanizidi shoga yangu
Kwa uzuri hujanzidi mimi
Kwa utamu hujanzidi shoga yangu
VERSE
Na huyo baby wako alikuwa wa kwangu
Kabla ya kuwa wa kwako
Hauniambii kitu kuhusu yeye
Hata kulala, alilala kwangu, kabla ya kulala kwako
Kwahiyo hunitishi mbwa wewe
Oya weh, hakuna ulichonizidi cha kunipa stress
We nyota yako ya kuni, mie mwenzako ya gesi
Mwenzako uzuri wangu natural sio wake wa kufeki
Maana mwenzangu una rangi nyingi ka' combati ya jeshi
PRE-CHORUS
'Asa mbona unapata tabu kujichubua
Tako huna unaforce kujibinua
Baby wangu hajadata na chura ka' hujajua
Kadata na mambo matamu 'nayomgea, nikwambie wewe
CHORUS
Kwa uzuri hujanizidi mimi
Kwa utamu hujanizidi shoga yangu
Ooh! Kwa uzuri hujanizidi mimi
Ai udugu we kwa utamu hujanzidi shoga yangu
Haunitishi hunisumbua (hujanizidi
mimi)
Jiangalie kuvaa hujui (hujanizidi shoga
yangu)
Ay! Hapo kwanza nicheke, haaa!
HOOK
Wanangu bado sijaskia shangwe kama umeme umerudi (huoo!)
Masela bado sijaskia shangwe kama umeme umerudi (huoo!)
Ay! Mara tena umekata (aah!)
Mama, mara tena umerudi (huoo!)
Wewe, mara tena umekata (aah!)
HOOK
Twende, show me gidi, gidi, gidi
Baby gidi, gidi, gidi
Twende gidi-gidi-gidi, gidi we
Gidi, gidi, gidi
VERSE
Kwanza muone amepandwa na ibilisi
Alikaa pembeni, hivi sasa ameingia kati
Ona mwili mkubwa kumbe kibonge mwepesi
Kulia kushoto, dunda kama kitenesi
HOOK
Twende sasa gidi, gidi, gidi
Gidi, gidi, gidi
Twende gidi-gidi-gidi, gidi
Gidi, gidi, gidi
Hapo kwanza nicheke, hahaaa!
VERSE
Oya we! we hili goma noma kwani amelipiga nani
Maana inafanya wanangu mpaka wanapandwa shetani
We hili goma noma kwani amelipiga nani
Maana wanavua mashati kwenye miti wanachuma majani
Oya wanachuma majani
Wanaleta majani mama
Wanachuma majani
Wanaleta majani oya
HOOK
Diblo nipe, nipe tena
Diblo nipe (DJ Kidogodogo) nipe tena
OUTRO
(Kamix Lizer)