
Tuma pesa Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:2020
Lyrics
Nimekutumia ujumbe asubuhi
Sababu gani hujajibu sijui
Nimekupigia mara kumi na mbili
Ni kama wanipimanisha akili
Kukopa kwako kweli ni harusi
Kulipa deni kwako ni matanga
Waniogopa mie kama virusi
Na sio vita me sijabeba panga
Tuma Pesa, tuma pia ya kutoa
Tuma Pesa, tuma mie nakungoja
Tuma Pesa, tuma pia ya kutoa
Tuma Pesa, tuma mie nakungoja
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
Aaah, mamama
Nimeshinda nikitazama simu yangu
Nakusubiri kwa hamu na gamu
Si ulisema ningoje wiki tatu
Na sasa zimepita miezi tatu
Kwenye magroupu unatuma meme
Meseji zangu unaweka blutiki
Kama ni ngumu rafiki si useme
Nijipe shuguli zangu za muziki
Tuma Pesa, uma pia ya kutoa
Tuma Pesa, tuma mie nakungoja
Tuma Pesa, uma pia ya kutoa
Tuma Pesa, tuma mie nakungoja
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
(Aaah, aaah, aaah, mamama)
Aaah, mamama
Tuma saa hizi (Tuma Tuma)
Tuma nipate usingizi
Tuma nitumie wazazi
Niwanunulie viazi
Tuma nitumie mama watoto
Aliteta eti ako musoto
Tuma pia me nijivinjari
Marafiki tunyoroshe whisky
Tuma tumaaaaaaa
Tuma tumaaaaaaa
Tuma tumaaaaaaa
Tuma tumaaaaaaa
Tuma tumaaaaaaa