Mchungaji Mwema (Upo) ft. Willybert Baraka Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2024
Lyrics
Bwana Mchungaji wangu
Sitapungukiwa na kitu
Wanilaza kwenye majani mabichi
Waniongoza kwenye maji matulivu
Wahuisha nafsi yangu
Kuniongoza kwa njia za haki
Nipitapo kwenye bonde la mauti
Sitaogopa hata ikiwa mabondeni
Upo bwana upo, na mabonde yanatii sauti yako
Nikienda milimani
Upo Bwana Upo
Na milima inatii sauti yako
Nikiwa kwenye giza
Upo Bwana Upo
Na Giza linatii mwangaza wako
Nikiwa mawimbini
Upo Bwana upo
Na mawimbi yanatii sauti yako
Mchungaji awachaye wale tisini na tisa
Kuniokoa ni wewe
Baba amkaribishaye yule mwana mpotevu, na kumvisha ni wewe
Mchungaji awachaye wale tisini na tisa
Kuniokoa ni wewe
Baba amkaribishaye yule mwana mpotevu, na kumvisha ni wewe
Tu Bwana, ni wewe
Ni wewe
Tu Bwana, ni wewe
Nikiwa mabondeni
Upo Bwana upo, na mabonde yanatii sauti yako
Nikienda milimani
Upo Bwana Upo
Na milima inatii sauti yako
Nikiwa kwenye giza
Upo Bwana Upo
Na Giza linatii mwangaza wako
Nikiwa mawimbini
Upo Bwana upo
Na mawimbi yanatii sauti yako
Watawala
Watawala
Mchungaji mwema eh
Watawala
Watawala
Watawala
Mchungaji mwema eh
Watawala
Halleluyah
Halleluyah
Mchungaji mwema eh
Halleluyah
Halleluyah
Halleluyah
Mchungaji mwema eh
Halleluyah
Mchungaji mwema eh
Halleluyah