![Safari ya maisha yangu ft. Steven Kanumba](https://source.boomplaymusic.com/group10/M00/04/29/5939b79562124d1ba98c290d72f3ad95_464_464.jpg)
Safari ya maisha yangu ft. Steven Kanumba Lyrics
- Genre:Spoken Word
- Year of Release:2004
Lyrics
Safari ya maisha yangu ft. Steven Kanumba - Bongo Records
...
Tangu Zamani baba yangu alinifundisha kuwa
Mtoto ni mtu mzima anayekua
Na mtu mzima ni mtoto aliyekua
Hivyo wajibu wa mzazi
Ni kumuandaa mtoto kua mtu mzima
Hapo muda wake utakapofika
Nyumbani kwetu hapakua na mahali pazuri kimaisha
Lakini baba yangu alinipa matumaini kua
Kama nitashika maelekezo yake ipasavyo
Hali hiyo itakuja kua historia
Nilikua nachunga mifugo ya nyumbani kwetu
Kwa bidii zote nikijua huu ni wajibu wangu
Tazama mifugo hii inavyopendeza juu ya uso wa dunia
Inaonyesha kila dalili za utulivu,amani na upendo duniani
Hainan Shambala wala haina mtaji
Lakini inaishi kwa matumaini na amani
kwa kumtumainia mungu muumba
Matumaini yalianza kuingia dosari
Wakati baba alipotutoka ghafla kwa ajali mbaya ya Gari
Kwa mujibu wa mafunzo ya baba
Mimi ingawa nilikua na umri mdogo
Nilijikuta nikiwa kiongozi wa familia
Nililazimika kufanya bidii zote
Kuhakikisha kua mdogo wangu Anita hapati tabu
Ila nilikosa kitu Kimoja tu
Maneno ya hekima ya baba
Kuanzia hapo nilikua nimepoteza uchangamfu kabisa
kwa kuwa sikua na sehemu ambapo
Nitapata matumaini mapya kuhusu maisha
Ila nilijua kua natakiwa kuhakikisha hali hii ya maisha
Itaondoka na tunaishi maisha mazuri kama wengine
Niliendeleza juhudi za kuchunga mifugo Na hata pale
Mifugo yetu ilipokubwa na magonjwa ya kutoweka
Nilikua nachunga mifugo ya watu wengine kwa ujira
Ilimradi tu maisha yasonge mbele
Nilikua eneo la malisho kila nilikua Nina muda
Nilifanya hivyo bila kuchoka kabisa.