Namba Yako Ninayo ft. P Mawenge Lyrics
- Genre:Hip Hop & Rap
- Year of Release:2024
Lyrics
Oiiiiiiih....
Hehehehe!!
DollSouth Baby!!
Mtusafi Again.
Na perfect
BoyMtusafiii
Okey
weeenge...
Perfect Kamix...
Oya wee si unaitwaga adili
Tumesoma shule moja kule kwetu primary
Iringa, Nyanzwa kwetu pagumu,
Hivi umenisahau mimi naitwa Salim
Unanipita mwanangu kama hunijui
Basi ungetisha angalau hata sumuni
Kwani ni vita udugu kama hunioni
Aaaaaahh, Umaskini kichomi
Tuseme nini namba yangu ndo uliipoteza
Au ndo vile sababu me sina fedha
Ni nene nini unadhani nilipoteza
Nikikusalim unanijibu kingereza.
Namba yako ninayo
Sasa mbona hunipigii?
Namba yako ninayo
Na mimi unipe madili?
Namba yako ninayo
Tafuta hela tu, namba yako ninayo!.
Aaaaaaaaaaaaaaaaahhh!!.
Namba yako ninayo
Unanitenga sana!.
Namba yako ninayo
Basi fanya unipigie!.
Namba yako ninayo
Apige nani wakati unapiga miayo!!.
Me nakukumbuka Fresh wala sijakusahau,
Tumekuwa wote sasa kivipi nikudharau
Me kuwa Fresh haimaanishi nimepanda dau
Sina pesa nyingi japo Life kidogo angalau.
Amka mwana kama muda mbona bado unao
Au unangoja dingi avute ufuatilie mafao
Hicho kipindi umejibweteka unacheza bao
Me ndo niko Race nabadili venue za vikao.
Heshimu sana muda mana ni kitu cha msingi
Tunazeeka sasa na tumeshakuwa madingi
tukimbizane kwenye mishemishe za shilingi
Ila ukizubaa ndugu utazidi kukata ringi
Juzi tulipishana upo kwenye kibaiskeli
Sikuisikia salamu ukadhani nakukejeli
Usikate tamaa mwana bado haujafeli
Chakalika fanya kazi kesho tukutane sheli
Namba yako ninayo
Sasa mbona hunipigii?
Namba yako ninayo
Na mimi unipe madili!.
Namba yako ninayo
Tafuta hela tu namba yako ninayo!!.
Aaaaaaaaaaahhh
Namba yako ninayo
Unanitenga sana!.
Namba yako ninayo
Basi fanya unipigie!.
Namba yako ninayo
Apige nani wakati unapiga miayo!!.
Hahahahahahaha!!
Oyaah wanangu eeeeh
Tutafute wazee
Mmemuona mwana alivyoniambia
Sasa sio kwa washkaji tu,mpaka familia
Kwenye vikao vya familia
Weee utakuwa unaambiwa tu
Na mwisho wa siku
Utakuwa unatumwa soda kwenye vikao
Utatumwa sana soda mzee
Mana kuna kushirikishwa
Halafu kuna kupewa taarifa
Sasa wewe utakuwa utakuwa unapewa taarifa mzee
Boymtusafiii..
Namba yako tunayo tafuta hela!.
Magembe Music Baby!!.