SAFISHA NJIA Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
SAFISHA NJIA
Verse 1
Mimi ni mdhaifu
Siwezi kutembea,
Nimebeba mzigo mzito,
Sijui ni nani atanitua,
Nimesikia leo,
yupo mtu anaeweza
kunitua mzigo wangu,
Yesu naomba nionane naye.
Verse 2
Nguo zangu Ni chafu
Siwezi jisafisha
Hata mwili huu wa udongo
Naona hauna thamani tena
Kweli ninayo haja
Kuonana naye saasa
tabibu na mwokozi wangu
Yesu naomba anitakase.
Chorus
Safisha njia Ili niipite
Nataka kumwona mwokozi kwanza
Nizunguze naye kwa kina,
Nimweleze ya moyoni mwangu,
Suluhisho pekee lililobaki
Ni NENO lake na Upendo wake
Neema yake Rehema zake
Msamaha vitaniokoa
Verse 3
Macho yangu dhaifu
Siwezi ona mbele
Hata Baraka nil'opewa
Sioni ni Kama zimejificha
Tazama Leo nimekuja
Kufunguliwa macho yangu yaone
Nataka kumwona Bwana
Leo haja yangu isikiwe
Chorus
Safisha njia Ili niipite
Nataka kumwona mwokozi kwanza
Nizunguze naye kwa kina,
Nimweleze ya moyoni mwangu,
Suluhisho pekee lililobaki
Ni NENO lake na Upendo wake
Neema yake Rehema zake
Msamaha vitaniokoa
Chorus (unison)
Safisha njia Ili niipite
Nataka kumwona mwokozi kwanza
Nizunguze naye kwa kina,
Nimweleze ya moyoni mwangu,
Suluhisho pekee lililobaki
Ni NENO lake na Upendo wake
Neema yake Rehema zake
Msamaha vitaniokoa