
Wimbo Wetu Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2023
Lyrics
Sijawai penda kupanda ndege
Hakuna kitu kitafanya nizoee
Nina hofia urefu sio siri
Ninatetemeka nikisafiri
Lakini hii kazi nimechagua
Najua itabidi nitembee
Mara nyingi itaturusha
Pande tofauti za dunia
Ikifanyika, simu nitachukua
Ili nisikize wimbo
Inirudishe Kando yako
Na nitakupigia, sauti nikisikia
Nitajihisi Niko kwako
Ukinihitaji hapo
Nitakukumbusha
Unaweza cheza wimbo wetu
Cheza ni wimbo wetu
Ukinihitaji we' icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu
Huu ni wimbo wetu
Nakumbuka usiku juzi juzi
Umelala Kando yako mpenzi
Nafasi ni kubwa kitandani
Umechagua Pande yangu lakini
Na Nikikuangalia
Jinsi umetulia
Nilijazwa na Raha hii ni baraka
Sana
Nikajipata, karatasi nachukua
Nikuandikie wimbo
Nikuanikie roho
Ukiamka, afathali utajua
Nakupa penzi dabo dabo
Ukinihitaji hapo
Nitakukumbusha
Unaweza
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Ukinihitaji we' icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu
Uuu - uuuh
Ukihitaji
Nikuwe nawe
Wewe icheze icheze
Oooh, wetu
Cheza wimbo wetu
Ukinihitaji we' icheze
Wakati wowote
Cheza wimbo wetu
Cheza wimbo wetu
Hata nikiwa mbali aje
Nitakuwa na wewe
Kwa wimbo wetu
Huu ni wimbo wetu