
Mungu Wa Mataifa Yote Lyrics
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2023
This song is not currently available in your region.
Try the alternative versions below.
Alternative versions:
Lyrics
Aah Aah , Aah Aah , Aah Aah ,
Ndiye Mwamba !
AHUU!
Ngai Ngai WaEmbu na WaKikuyu, wanamuita hivyo
Enkai Enkai Maasai wanashujudia, AHUU!
Eeh,
Ni Mungu mmoja tunayemuabudu
Hana mipaka wala hana kabila
Ni jana leo hata milele,
Wakenya wote tumuinue
Wajaluo wamuite ; Nyasaye
Wakipsigis ; Cheptalel
Abakuria; Nokwe
Waluhyia wamuite ; Were
Wateso wanamuita Adek
Mmh, Wazungu mpaka Afrika
Warabu na hata India
Ukifika kule utapata majina
CHORUS
Ni Mungu wa mataifa yote,
Ni Mungu wa makabila yote ( ×2 )
Wanyama na ndege wanamuita pia
Dunia yote tumshujudu Mungu
Kwa vilugha vya malaika na mataifa
Kwa lugha ya ishara tuonyeshe
Kwa Kiganda nimuite Katonda wange
Samburu wamuite Nkai
Mulunguuu, Wakamba na Wagiriama,
Wataita na Wamijikenda, wanamuita Mungu hivyooo
Enkoro ni Abagusi na Wakisii
Waturkana wamuite Akuj
Wapokot wamuite Tororok
Apak , Iteso wanavyomuita
Waq , Randile na Borana
Saboat , Kalenjin na Wanandi wanamuita Asis
Mmhhh
Na wanapomuabudu Wameru wanamuita Murungu
Allah ni Mungu wa Kiarabu
Illahi Mungu wa Somali
" Dieu ni Mungu kwa Kifaransa, Aaah!"
CHORUS
Ni Mungu wa mataifa yote,
NI Mungu wa makabila yote ( ×2 )
Ita Mungu kwa kilugha ya kikwenu
Ita Mungu kwa kilugha ya kikwenu
Basi sifu Mungu kwa kilugha unayojua
Sifu Mungu kwa kilugha unayojua
CLIMAX
All: Yaweeh we ni Mungu wa wote
Yaweeh we ni Jehovah
SOLO: Kwenye mnara wa babeli
Ulitofautisha lugha
Ili wakusifiee
Na Wazungu, Wahindi na Warabu wotee
wanakushujudu Baba heee
We wa wotee, we niwa wotee
Eeh Mungu, Eeh mungu weeeh
Kusini na magharibi, mashariki kaskazini
Kila mahali
Makabila yotee Baba
Hauna ubaguzi wowoe
Kwa vilugha nitakuimbia mpaka vilugha vya
malaika
Eeeehh Baba
Ni wewe Bababaababaaa
Ni Jehova, ni Jehovah
Yelelelee
Mataifa yotee