
Maisha Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2019
Lyrics
Maisha haya ni safari, yahitaji moyo
Yatupasa kujikabidhi kwake Bwana wa upendo
Ndipo maisha haya, yatakuwa salama
Tutakapojiwe kwa Yesu wa maisha
Vikwazo vingi safarini vyaumiza moyo
Wengi twapoteza imani kwake Bwana wa upendo
Huwezi kwendelea, na hofu ya maisha
Pasipokujiweka kwa Yesu wa maisha
Tembea na Yesu, ongea na yeye tu, utakuwa salama kwa Yesu wa maisha
Tembeana Yesu, ongeana yeye tu, utakuwa salama kwa Yesu wa maisha
Pasipokujiweka kwa Yesu wa maisha
Utakuwa salama kwa Yesu wa maisha