Vibaya Lyrics
- Genre:Others
- Year of Release:2023
Lyrics
Sura unavi dimpodimpo
Moyo wangu taabani kwako
Mwambie bado niponipo
Penzi naezeke na kokoto
Nikutoe out foradhani
Tuwe wote tujenge ramani
Wakiteta kwetu burudani
Penzi limewazidi uzani
Mi na wewe vanesa rotimi
Dua zetu yassini watini
Shida raha we baki na mimi
Eehhh yeeh
Mi na wewe vanessa rotimi yassini watini
Shida raha we baki na mimi
Nitajihisi vibaya tukitengana
Nitajihisi vibaya tukipotezana
Nitajihisi vibaya tukitengana
Nitajihisi vibaya tukipotezana
tukipotezana
Pendo langu sukari guru moyo wangu zawadi nakupa
Tena beba bila ushuru ukiweza nitupe kimboka
Mana sura yako (kama malaika wa peponi)
Mi mwenzako (umenikaba rohoni)
Acha waseme watupige mawe
Na popote nitakwenda nawe
Penzi tulijaze choyo tupendane wawili tu
Kama muziki tucheze sebene
Najikoni ugali senene
Penzi tulijaze choyo tupendane wawili tu
Mi na wewe vanesa rotimi
Dua zetu yassini watini
Shida raha we baki na mimi
Eehhh yeeh
Mi na wewe vanessa rotimi yassini watini
Shida raha we baki na mimi
Nitajihisi vibaya tukitengana
Nitajihisi vibaya tukipotezana
Nitajihisi vibaya tukitengana
Nitajihisi vibaya tukipotezana
Oooh my ooohh my oooh