![Shida Pt 1& 2](https://source.boomplaymusic.com/group1/M00/52/60/rBEeMVn4Q8eAQCCxAABhUoACfv8802.jpg)
Shida Pt 1& 2 Lyrics
- Genre:Afrobeats
- Year of Release:1970
Lyrics
Shida Pt 1& 2 - Mbaraka Mwinshehe
...
Hakuna kitu kibaya sana humu duniani kama shida
Haichagui mtu, siku wala mwaka
Haina katu taarifa shida huingia shida bila hodi
Si mtoto wala mkubwa wote shida
Kila siku shida shida haiishi mpaka siku ya mwisho.
Shida kamwe haikosekani hata kama siku ya harusi
Na uwe na mapesa mengi ipo shida
Haina ngoja wala haibu popote shida hutokeza
Kwa masikini matajiri wote shida
Kila siku shida shida haiishi mpaka siku ya mwisho.