NIKAFATE NINI Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Vase 1
Ile siku nagombana na mke wangu,
ghafla nageuka nyuma eeh,
nawaona majirani wanafurahi
Ile siku ya matatizo tele kwangu
ooh nageuka nyuma eeh
naona rafiki zangu wanafurahi.
Ile siku ninafukuzwa kazi ooh
nageuka nyuma mimi
wenzangu wanafurahi iiih
Ile siku nimetolewa vyombo nnjee
nimeshindwa kulipa kodi
ndugu zangu wanafurahi iiih
Lakini Mungu ni wewe pekee
uliyebaki na mimii kipindi chotee × 2
Chorus
Wanasema nimfate shetanii
( nikafate nini ukoo ) Munguu
( nikafate nini ukoo ) Munguu
( Nitabaki na wewe milelee )
Vase 2
Ile siku nipo hospitali nimezidiwaa
walewale wote simu zao hazipatikanii
Ile siku nimesingiziwa kesi
nikapelekwa segerea
yani wote hawajaja kuniona
Ile siku narandaranda mitaani
kutafuta kibaruaa wananichekaa
ile siku biashara imekufaa
Mtoto wangu masomo kakatishwaa
heee wananichekaa
Lakini Mungu ni wewe pekee
uliyebaki na mimii kipindi chotee × 2
Chorus
Wanasema nimfate shetanii
( nikafate nini ukoo ) Munguu
( nikafate nini ukoo ) Munguu
( Nitabaki na wewe milelee )