Jiamini (feat. ROSE MUHANDO) Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2022
Lyrics
Jiamini (feat. ROSE MUHANDO) - UPENDO MWANGUPILI
...
lyric sync by Phellow 254790511905
****chorus*****
Jiamini
utatenda mambo makubwa
jipe moyo
unaweza kama wengine
Jiamini
utatenda mambo makubwa
jipe moyo
unaweza kama wengine
****verse1*****
Mungu amemuumba yule
amekuumba na wewe
al'ompandisha yule
atakupandisha na wewe
al'ombariki yule
atakubariki na wewe
jiamini
acha hofu
jiamini
jiamini mama
unaweza kama wengine
ai
jipe moyo
mama jipe moyo
unaweza kama wengine
al'ompa magari yule
atakupa na wewe
Mungu al'omuumba yule
amekuumba na wewe
al'omuheshimu fulani
atakuheshimisha na wewe
jiamini
kama simba jiamini
unaweza kama wengine
*****chorus******
Jiamini
utatenda mambo makubwa
ondoa hofu maishani mwako mama jipe moyo
jipe moyo
usihofu jipe moyo simama
unaweza kama wengine
simama imara jipe moyo jitie nguvu
Jiamini
simama imara na wee ah
utatenda mambo makubwa
kwa nini ukate tamaa wakati Mungu yuko upande wako?
jipe moyo
acha kulia jipe moyo
unaweza kama wengine
*****verse2*****
una nini Mikononi mwako mama?
je, umeshika nini mkononi mwako wewe?
una fungu la mchicha mkononi mwako wewe
waendesha bodaboda Mikononi mwako wewe
unauza mihogo mikononi mwako mama
unatembeza ndizi mkononi mwako wewe
fimbo ya Musa kidogo tu
ilimeza majoka ya Farao
fimbo ya Musa kidogo tu
iligawanya bahari ya Shamu
una nini mkononi mwako mama?
una nini mikononi mwako wewe
yule ana kampuni alianza kama wewe
ona tajiri mkubwa alikuwa kama wewe
anaendesha gari
alianza kama wewe
tatizo haliko kwenye utendaji wako
tatizo liko kwenye akili yako
tatizo haliko kwenye mikono yako
tatizo liko kwenye akili yako
woga wako ndio umasikini wako
kadri ulivyofikiri ndivyo ulivyokuwa
kadri ulivyofikiri ndivyo ulivyo leo
jiamini
unaweza kama wengine
yemamamamamamamama!
******chorus*******
Jiamini
jipe nguvu
utatenda mambo makubwa
nasema usiogope macho yao jitie nguvu inuka wewe
jipe moyo
unaweza kama wengine
Mungu aliyemuumba yule ndiye aliyekuumba na wewe
Jiamini (mama jiamini) (bodaboda jiamini)
utatenda mambo makubwa
mamatilie jipe moyo jivike nguvu
jipe moyo
halalalala iyeeeeeeee-aaaaah!
unaweza kama wengine
lyrics synchronised by Phellow 254790511905