
Mtu Huru
- Genre:World Music/Folklore
- Year of Release:2015
This song is not currently available in your region.
Lyrics
Mtu Huru - Mrisho Mpoto
...
Ardhi yenye afya imebeba watu wadhaiiifu! watu dhaifu wamebeba utukufu eeh Bora ukapime ujue uwe huru twende ukapime ujue uwe huru Zama zile Bwana kufuli alipoitoka dunia sababu zilikuwa zimeekwa mezani Umaskini , hakuna elimu kafa tena Bin Skununu sababu zimemwaga sebuleni hila zake zimemwondoa hehehehe Haya Jana katoroka kijana mwingine mshaandika risala ukapela uooo iweje upo upo tu ona yamemkuta hamwishi vijisababu jamani sasa leo katutoka mister smart punde tutakula ubwabwa na kwenda zetu tubwie bia na mapochopocho tukasimuliame mbele uko wanao wamebaki wamejikunyata kama vifaranga vya kuku mkewe Mamsap amebaki na kizunguzungu chake huyu je hamna vijisibabu najua mmeishiwa wasifu wake mimi nitawapa alikuwa mtanashati elimu si ya manati chuo kikuu ametamati madaraka mezani pesa chekwa chekwa magari lukuki nyumba usipime eeeh sasa vimepenyaje tena uko ndugu yangu wa damu katika vicheko hivi kuna maumivu zama kina upate ukweli upate sababu ya dhati sio chati sababu ya kweli hukupa jibu la kweli . Ardhi yenye afya imebeba watu wadhaifu watu dhaifu wamebeba utukufu Bora ukapime ujue uwe huru twende ukapime uwe huru Tangu unajua toka nikwambie siku ile uwende ukapime umepoteza raha na mie ndugu yako hii si ajabu lakini wewe uwe tofauti na wengine vunja mwiko wa uoga uwe mtu huru mtu ajuae hali yake ndugu yangu kujua hali yako ni sehemu ya ushindi twende ukapime fikiri kuhusu mashaka uliyonayo ukipata mafua unaugua mara mbili ukipungua uzito kwa ajili ya kufururiza night na kutokula vizuri unachanganyikiwa kwa kuwa hujijui Shija alipopima alihisi ameutua mzigo mzito sana alikutwa na virusi na rafiki yake Mzinga hakuwa navyo unasihi wa wataalamu ulimpa nguvu na hali ya kuishi embu fikiri ndugu yangu Mzinga miaka sita baadae kafa kwa kisukari Boss wake aliyempunguza kazi amefariki kwa vidonda vya tumbo lakini yeye ana afya timamu ameongeza elimu yake ameongeza kipato na rasilimali ametengeneza ramani ya maisha yake yani ana dira ni heri ndugu yangu usipokuwa na virusi lakini ukikutwa navyo si mwisho wa uhai kwani mapambano utayamiliki ndugu yangu twende ukapime wewe wajua kuwa Jacob anaishi na virusi mwaka wa ishirini sasa alitaka kujiua kwa hofu mwaka wake wa kwanza Shangazi yake akamwambia awe na subira amesubiri na je dawa ya UKIMWI ikigundulika kesho haitakuwa heri yake aliyesubiri ndugu yangu usipojijali utawakosea wengi sana Mungu wako aliyekupa uhai ambao ukitoka haurudi familia yako uliyoapa kuipenda na kuilinda marafiki zako wanaokumiss usipokuwepo taaluma yako uliyowekeza na nguvu zako na muda wako kujifunza kwa umma wote unaotegemea huduma zako kwa taifa lako tukufu pia ebu anza leo kujali na kujua afya yako ndugu uingie kwenye chama cha watu huru twende eeh Ardhi yenye afya imebeba watu wadhaifu watu dhaifu wamebeba utukufu Bora ukapime ujue uwe huru twende ukapime ujue uwe huru, ndugu yako rafiki nakupendaaaah twende ukapime ujue uwe huru usikate tamaa usikate tamaa twende ukapime ujue uwe huru twende twende usikate tamaa Lyrics by Mpindu_brand
Similar Songs
More from Mrisho Mpoto
Listen to Mrisho Mpoto Mtu Huru MP3 song. Mtu Huru song from album Waite is released in 2015. The duration of song is 00:05:44. The song is sung by Mrisho Mpoto.
Related Tags: Mtu Huru, Mtu Huru song, Mtu Huru MP3 song, Mtu Huru MP3, download Mtu Huru song, Mtu Huru song, Waite Mtu Huru song, Mtu Huru song by Mrisho Mpoto, Mtu Huru song download, download Mtu Huru MP3 song
Comments (2)
New Comments(2)
haki ally
DAVID IBRAHIMnp7vs
nzuri
noma